DC SENDIGA AWATAKA WACHIMBAJI KUCHANGAMKIA BIMA YA AFYA

Na Mwandishi wetu, Mirerani. 

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amewataka wachimbaji wa madini wa eneo hilo kuchangamkia bima ya afya kwa wote ili waweze kupatiwa huduma za matibabu pindi wakiugua. 

RC Sendiga ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama wachimbaji cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara MAREMA uliofanyika kwa muda wa siku mbili Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro. 

Ameeleza kwamba wachimbaji madini wa mkoa huo wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo ya bima ya afya kwa wote.

Amesema bima ya afya kwa wote unachangia shilingi 150,000 kwa mwaka na unapatiwa huduma za afya kwa kaya ya watu sita wakiwemo baba, mama na watoto wanne. 

"Wachimbaji madini mnapaswa kuchangamkia hii fursa kwani unakuwa na uhakika wa kupata matibabu wewe na familia yako pindi mkihitaji huduma na hamtapungukiwa na kitu na kununiana kutaisha," amesema RC Sendiga.

Ameeleza kwamba hivi sasa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeshawaandalia makundi yasiyojiweza wakiwemo wazee kupata matibabu kupitia bima ya afya. 

Hata hivyo, Mwenyekiti wa MAREMA Elisha Nelson Mnyawi amemuhakikishia RC Sendiga kuendelea kutoa elimu kwa wachimbaji ili wajiunge na bima ya afya kwa wote. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.