Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 25, 2026

VIKUNDI 222 UYUI VYAWEZESHWA MIKOPO NAFUU YA BILIONI 1

Picha
   Na Allan Kitwe, Tabora. HALMASHAURI ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora imetoa mikopo nafuu isiyo na riba ya shilingi bilioni 1 kwa vikundi 222 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo ili kuwainua kiuchumi. Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi za mikopo hiyo jana, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo Amoniche Mtweve amesema kuwa mikopo hiyo imetokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri. Ameongeza kuwa jumla ya wanachama 1,121 wanaounda vikundi hivyo wamenufaika na mikopo hiyo na kuwapa nguvu ya kuendeleza miradi yao ya biashara na uzalishaji mali katika maeneo yao. Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Shabani Katalambula, amewataka wanufaika kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwezesha wananchi wengine kunufaika na mikopo hiyo katika awamu zijazo. Amefafanua lengo la mikopo hiyo kuwa ni kusaidia vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi kupitia miradi midogo midogo ya ujasiriam...

MADIWANI TABORA WAPEWA MAFUNZO YA UWAJIBIKAJI

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora MADIWANI wa halmashauri ya manispaa Tabora na Uyui Mkoani Tabora wamepewa mafunzo maalumu yatakayowawezesha kutekeleza wajibu wao kwa weledi mkubwa kwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni. Akifungua mafunzo hayo leo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tabora Mohamed Katete amesema kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati mwafaka baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ili kuwajengea uwezo. Amebainisha kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa kuwa yatawaongezea weledi katika kusimamia utendaji wa halmashauri zao na kuongeza kasi ya kutumikia wananchi waliowachagua katika kata zao. ‘Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mafunzo haya yatolewe kwa madiwani wote nchini ili kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa weledi mkubwa na kukamilika kwa wakati’, ameeleza. Aidha amewataka kujenga mahusiano mazuri na wataalamu na watendaji wa halmashauri zao na kuhakikisha fedha zinazoletwa na serikali kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo na z...

RAIS SAMIA AMEING'ARISHA SIMANJIRO - DC LULANDALA

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro.  MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mwalimu Fakii Raphael Lulandana ameeleza kwamba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeing'arisha Simanjiro kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo. DC Lulandala akizungumza mji mdogo wa Orkesumet makao makuu ya Wilaya hiyo amesema Rais Samia katika kipindi kifupi cha utawala wake amefanikisha maendeleo mengi katika eneo hilo. Ameeleza kwamba kwenye sekta ya nishati ya umeme hivi sasa vijijini vyote 56 vya Wilaya ya Simanjiro vina huduma hiyo ikibakia vitongoji vichache ambavyo navyo vitafungiwa umeme. "Wakati Rais Samia anaingia madarakani katika Wilaya ya Simanjiro ni vijiji 21 pekee ambavyo wananchi wake walikuwa wanapata nishati ya umeme," ameeleza DC Lulandala. Amesema hata baadhi ya watu wa Simanjiro waliodanganywa na baadhi ya wanasiasa kuwa maeneo yao yataporwa na kugeuzwa kuwa mapori tengefu na mapori ya akiba niliwaeleza wasiamini hayo. "Rais Samia haw...

FCT YAENDELEA KUWAWEZESHA WADAU ARUSHA KUPITIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Arusha. BARAZA la Ushindani (FCT) limewahimiza wadau na wafanyabiashara mkoani Arusha kutumia kikamilifu mfumo wa usajili wa mashauri kwa njia ya kielektroniki (e-filing), lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na kupunguza gharama katika uwasilishaji wa mashauri. Akizungumza katika mafunzo hayo Msajili wa Baraza hilo, Mhe. Mbegu Kaskasi, alisema mfumo huo wa kisasa umeundwa ili kurahisisha usajili wa mashauri na rufaa bila wadau kulazimika kufika katika ofisi za FCT, hatua ambayo itaokoa muda na kuongeza ufanisi. “Mfumo huu utaimarisha uwazi, kasi ya utoaji haki na kupunguza usumbufu kwa wadau,” alisema Mhe. Kaskasi, akibainisha kuwa hatua hiyo inakwenda sambamba na msukumo wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma."amesema Mhe.Kaskasi. Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Moses Pesha, amelipongeza Baraza kwa kuendelea kutoa elimu kwa wanaohusika na wananchi kwa ujumla, akisema hatua hiyo imeongeza ...