Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 17, 2025

DIAMOND AMJIBU BABA LEVO NA MBOSSO.

Picha
STARA wa Bongo Fleva, @diamondplatnumz , ameweka wazi msimamo wake kupitia ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akieleza kutofurahishwa na mwenendo wa rapa Baba Levo juu ya Msanii @mbosso_ Diamond amesema anamuheshimu Baba Levo kama kijana mwenzake, lakini vitendo vyake vinamfanya ahisi kuna agenda asiyoijua, jambo linalomlazimisha kukaa mbali naye. #Diamondplatinumz #WCB #Babalevo #Mwijaku #Mbosso 

AJALI YA BASI.

Picha
BASI LA KAMPUNI YA MBEYA CITY EXPRESS LIMEPATA AJALI LEO 17.08.2025 ENEO LA CHIMALA.

MWENGE WA UHURU WAZINDUA DARAJA LA KINYANG'ERERE MARA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mara.  JUMLA ya shilingi Milioni 148.5 zimetumika Kujenga Daraja la kinyang'erere lililopo katika kijiji cha kinyang'erere halmashauri ya Musoma Mkoani Mara. Akisoma Taarifa ya ujenzi wa Mradi huo Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Musoma, Mhandisi Mohmed Etanga amesema daraja hilo limekamilika ujenzi wake kwa asilimia mia moja na kutoa huduma kwa Wananchi kama ilivyo kusudiwa. Mhandisi Etanga ameongeza kuwa daraja hilo ni kiungo muhimu kwa wakazi wa kijiji hicho kwaajili ya usafirishaji wa Mazao na kwenda kupata huduma za kijamii katika vijiji vingine ambapo kuna kituo cha Afya pamoja na wanafunzi kuvuka kwenda shule. Ameongeza kuwa kipindi cha Masika wakazi hao walikuwa wakipitia kadhia ya kushindwa kuvuka mto ambao unakuwa umejaa maji jambo lilikuwa likisababisha baadhi ya wajawazito kujifungulia njiani na kushindwa kuuza mazao yao kutokana na ubovu wa barabara . Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ndugu Ismail Ali Ussi ameipongeza TARURA kwa kufanya...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO TANZANIA.

Picha
TMA: Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24. 

DKT.MWINYI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR

Picha
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC,  kilichofanyika Afisi Kuu CCM Kisiwandui Zanzibar tarehe 17, Agosti 2025.

IDADI YA MAFUNDI WALIOOKOLEWA CHINI YA ARDHI MGODINI YAFIKIA SABA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Shinyanga.  Idadi ya mafundi waliookolewa baada ya kufunikwa na kifusi mgodini imefikia saba, baada ya Marko Ngelela (26), mkazi wa Sengerema na Machia Shabani (43) mkazi wa Ishokela mkoani Mwanza kuokolewa wakiwa tayari wamefariki dunia. Ajali hiyo ilitokea Agosti 11, 2025 katika mgodi wa Nyandolwa, wakati mafundi 25 walipokuwa wakifanya kazi ya ukarabati katika maduara matatu tofauti ambayo ni Na. 20, 103 na 106. Kwa mujibu wa taarifa za awali, ardhi ilititia ghafla na kusababisha kifusi kuporomoka, hali iliyowafunika baadhi ya mafundi waliokuwa kazini chini ya ardhi. Tangu tukio hilo kutokea, juhudi kubwa zimekuwa zikiendelea kutoka kwa timu ya uokoaji ya mgodi huo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, pamoja na wataalamu wa usalama wa migodini.  Hadi sasa, mafundi saba wamefanikiwa kutolewa chini ya kifusi, ambapo wanne kati yao waliokolewa wakiwa hai ambapo mmoja kati yao alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Kituo cha Af...