Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 11, 2025

UTAFITI MIAMBA BONDE LA EYASI WEMBERE WATHIBITISHA UWEZEKANO WA UPATIKANAJI MAFUTA

Picha
 *Dkt Mataragio akagua shughuli za utafiti na kutoa maelekezo kwa TPDC na AGS*   *Awamu ya  pili ya utafiti kukamilika Aprili 2026.*   *Asilimia 90 ya wanaotekeleza mradi ni watanzania*  Na Mwandishi Wetu, Arusha. UTAFITI unaofanyika katika  mradi wa kimkakati wa  Eyasi Wembere unaolenga kutafuta mafuta na gesi katika bonde la ufa la Afrika  Mashariki umeonesha matumaini makubwa ya kupatikana kwa Mafuta na Gesi katika bonde hilo. Hayo yamebainika wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa  mradi huo mkoani Arusha wilaya ya Karatu.  “Kazi za utafiti wa mradi huu zimeanza mwaka 2015,  tumekuwa tukikusanya data mbalimbali zinazohusiana na uwepo wa mafuta na gesi ambapo baada ya ukusanyaji, data hizo zilitumika kubainisha miamba tabaka ambayo ina mafuta na tukajiridhisha kwamba katika eneo hili la bonde  ipo miamba ambayo inaweza ikahifadhi m...

IGUWASA YATATUA KERO YA MAJI SHULE YA MSINGI CHIPUKIZI B IGUNGA.

Picha
  Na Lubango Mleka, Igunga MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Igunga (IGUWASA) imefanikiwa kutatua tatizo sugu la maji katika Shule ya Msingi Chipukizi B iliyopo eneo la Mtaa wa Sanzura, Wilaya ya Igunga, Mkoani Tabora. Zaidi ya Wanafunzi 200 pamoja na Walimu na Wakazi wanaozunguka Shule hiyo  wameanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama, hatua inayotarajiwa kusaidia kudhibiti milipuko ya magonjwa na kuboresha mazingira ya kujifunzia. Wananchi waliozungumza na blogu ya Habari Kamili wakati wa zoezi la uchimbaji mtalo kwa ajili ya kulaza bomba la maji wamesema huduma hiyo ni faraja kubwa baada ya kusubiri kwa muda mrefu. Maria Luhende, Rajabu Juma, Aisha Mussa, Elias Kishiwa na Paul Joseph, ni baadhi ya wakazi wa mtaa wa Sanzura waliojitokeza katika zoezi la uchimbaji wa mtalo wameipongeza IGUWASA kwa kufanikisha mradi huo. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Stoo, Phabian Lushindika, amesema hatua hiyo ni ya kupongezwa na amehamasisha wananchi kushiriki katika kulinda m...