DAKTARI HATIANI KUUZA SARUJI NA MATOFALI ZAHANATI SUKURO
Na Mwandishi wetu, Simanjiro. MGANGA mfawidhi wa zahanati ya kijiji cha Sukuro kata ya Komolo wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Dk Daud Ndagala ametiwa hatiani kwa ubadhirifu wa mifuko ya saruji na matofali ya kukarabati zahanati hiyo. Mahakama ya wilaya ya Simanjiro imemtia hatiani Dk Ndagala kupitia shauri la jinai namba 4344/2026 kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi. Hakimu mkazi mkuu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Simanjiro Charles Uisso amesoma hukumu hiyo Machi 26,2026 na mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) kituo maalum cha Mirerani Gervas Sarakikiya. Hakimu Uisso ameieleza mahakama hiyo kuwa Dk Ndagala ametiwa hatiani kwa kufuja Sh1 milioni za mauzo ya mifuko 57 ya saruji ya kukarabati zahanati hiyo. Amesema pia, Dk Ndagala alichepusha tofali 220 zilizoandaliwa kwa ajili ya ukarabati huo kisha akaziuza Sh605,000 kwa mtu binafsi. Amesema mshtakiwa huyo amefanya makosa hayo akitumia nafasi yake ya mganga mfawidhi wa zahanati ya ...