UFAWAZA WAIPONGEZA DOREFA KWA USIMAMIZI NA UENDESHAJI SOKA DODOMA.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
UMOJA wa Wanamichezo wa zamani wa Mkoa wa Dodoma (UFAWAZA) umekipongeza Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA) chini ya Mwenyekiti Aden Mohammed kwa jinsi ambavyo kimekuwa kikiendesha na kusimamia kwa weledi soka la mkoa wa Dodoma.
Pongezi hizo zimetolewa leo Machi 28,2026 Jijini Dodoma na Mjumbe wa Ufawaza,Samson Mkotya wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa DOREFA.
Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu kutoka Wilaya za Mkoa wa Dodoma pamoja na Vyama shiriki.
Mkotya ambaye kitaaluma ni Mwalimu na Mwanasheria amesema DOREFA imefanya mambo makubwa katika soka la Mkoa huo ikiwemo kuhakikisha soka linachezwa kuanzia katika ngazi za madaraja ya chini.
"Kipekee naomba nikupongeze Mwenyekiti wetu (Aden Mohammed) tunajivunia wewe.Mkutano huu ni uthibitisho tosha mnatembea na Matukio kwa kuhakikisha Mikutano ya kikatiba inafanyika hakika mnalitendea haki soka la Dodoma,"amesema Mkotya.




Maoni