NDANI ya Jiji la Dar es Salaam au kwengineko ukiendesha kwa mwendo wa wastani wa kati ya 50-60Kph kwenye Zebra yoyote utaweza kusimama na kuwapisha wavukaji wavuke, ila spidi ikizidi hapo sio rahisi kusimama hasa mwenda kwa miguu anapotokea ghafla. Hata hivyo, Jizoeshe Kusimama kwenye kila zebra kupisha watu wavuke, maana hata wewe ni mwenda kwa miguu ukitoka kwenye usukani. Usiposimama kuwapisha, hawatakuwa na mahala pengine salama pa kuvuka zaidi ya kuhatarisha maisha yao. Hivyo jambo la kwanza ondoa ile kasumba au mtazamo kuwa *Aagh wasumbufu hawa*, kwakuwa hata wao hao unaowaona kero wana haki ya kutumia barabara. Ni tofauti ya kipato tu au mazingira ya wakati huo ndio yamewafanya kwenda kwa miguu. Na jinsi miji inavyozidi kukua ndivyo idadi ya watu inavyoongezeka huku kukiwa na miundo mbinu michache sana ya waenda kwa miguu, tegemea idadi kubwa ya waenda kwa miguu kila kwenye zebra. Hivyo kuwa mwenda kwa miguu sio dhambi. Hii ndio sababu k...