SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. MUSSA AZZAN ZUNGU (MB) ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MBUNGE WA PERAMIHO MHE. JENISTA JOAKIM MHAGAMA KILICHOTOKEA LEO 11,DESEMBA,2025 JIJINI DODOMA.
MWILI wa hayati Spika Mstaafu wa Bunge na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa Mhe. Job Justino Ndugai, umeshawasili katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma kwa ajili ya viongozi wa kitaifa, familia, wabunge na wananchi kutoa heshima zao za mwisho na baada ya hapo mwili wa hayati Job Yustino Ndugai utaelekea nyumbani kwake Kongwa Jijini Dodoma.
Na Mwandishi wetu, Simanjiro MWENYEKITI wa kijiji cha Namalulu Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, Marumai Kirikai amepumzishwa kazi kwa muda wa siku 28 ili kupisha uchunguzi wa matumizi mabaya ya madaraka katika kijiji hicho. Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Fakii Raphael Lulandala ameunda kamati ya watu saba itakayofanya uchunguzi kwa muda wa siku 24 na baada ya siku 28 endapo Mwenyekiti huyo atabainika hausiki na tuhuma hizo atarejea kwenye nafasi yake. Lulandala ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Namalulu, baada ya kusikiliza kero, malalamiko na changamoto zao. Ameeleza kwamba hamsimamishi kazi Mwenyekiti huyo ila anapisha uchunguzi kwa muda wa siku 28 na endapo hatakuwa na makosa atarejea tena kwenye nafasi hiyo. "Hausimamishwi kaz ila unakaa pembeni kwa muda wa siku 28 ili kupisha uchunguzi na ofisa mtendaji wa kijiji cha Namalulu Sarafina Olotu ataongoza kijiji kwa kipindi hiki," amesema DC Lulandala. DC Lulandala amewataja wajumbe saba wa kamati ...
Na Mwandishi Wetu, Tabora. HALMASHAURI ya Wilaya ya Igunga imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Mamlaka za Serikali za Mitaa (Tabora na Kigoma) wakati wa Maonesho ya Nanenane mwaka 2025 ngazi ya kanda yaliyofanyika Uwanja wa Maonesho Ipuli - Tabora. Aidha, imeshika nafasi ya pili katika kundi la washindi wa jumla wa mikoa ya Tabora na Kigoma wakati wa Maonesho hayo. Akizungumza baada ya Halfa hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Ndug. Elizabeth Rwegasira amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Selwa Hamid kwa ushirikiano mzuri na Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Grace Nyamwanji kwa kufanikisha ushindi huo. Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halamshauri hiyo, Grace Nyamwanji amewashukuru na kuwapongeza, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watumishi na Wadau wote waliyoshiriki maonesho hayo kwa sababu wao ndio chachu ya ushindi huo.
Maoni