Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 22, 2025

DKT. MATARAGIO AAGIZA VIFAA VYOTE VYA UHAKIKI WA JOTOARDHI ZIWA NGOZI KUFIKA KWA WAKATI

Picha
  Ni baada ya kukagua mradi na kukuta baadhi ya vifaa bado havijafika Asisitiza mradi kukamilika kwa wakati ikiwa ni  utekelezaji wa Sera ya Nishati ya mwaka 2015 Kazi ya uhakiki wa Jotoardhi Ziwa Ngozi yafikia asilimia 60. Na Mwandishi Wetu, Mbeya. NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni yake Tanzu ya Uendelezaji Jotoardhi (TGDC)  kuhakikisha kuwa vifaa vyote vya uhakiki wa rasilimali Jotoardhi  katika mradi wa Ziwa Ngozi  vinafika kwa wakati ili kazi za uhakiki  ziweze kumalizika kulingana na muda uliopangwa. Dkt. Mataragio ametoa maagizo hayo leo Oktoba 22, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua kazi zinazoendelea kutekelezwa katika mradi huo wilayani Rungwe mkoani Mbeya. “Huu mradi mnapaswa kuukamilisha kwa wakati kutokana na umuhimu wake nchini, tunapotekeleza miradi hii ya Jotoardhi tukumbuke kuwa tunatekeleza pia Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015 ambayo inasema Tanzania in...

WANAFUNZI WATAKIWA KUDUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mara. AFISA Ushirikishwaji Jamii Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Thomas Mapuli, Oktoba 22,2025 amekutana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mshikamano iliyopo katika Manispaa ya Musoma, ambapo ametoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia na umuhimu wa kutunza amani katika jamii. Akizungumza na wanafunzi hao shuleni hapo ACP Mapuli aliwasisitiza vijana kuwa mabalozi wa amani na kuzingatia maadili mema, huku akiwataka kujiepusha na vitendo vya vurugu, ubaguzi, na ukatili wa aina yoyote, ikiwemo ule wa kijinsia. Aidha, aliwahimiza wanafunzi kuzingatia masomo yao na kuepuka vishawishi vinavyoweza kuhatarisha ndoto zao za baadaye, akibainisha kuwa elimu ndiyo ngao kuu ya kupambana na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi. “Jamii yenye amani huanza na mtu mmoja mmoja. Ninyi kama vijana mna wajibu wa kuwa mfano wa kuigwa, kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya ukatili wa kijinsia, na kushirikiana na vyombo vya dola kutoa taarifa za vitendo hivyo pindi vin...

SERIKALI KUPITIA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI

Picha
Na Hamida Ramadhani, Dodoma. SERIKALI kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatarajia kuanza utekelezaji wa awamu mpya ya ujenzi wa minara 280 ya mawasiliano, ambapo baadhi ya minara hiyo itajengwa katika maeneo ya mipakani, mbuga za wanyama, na njia kuu za reli za SGR na TAZARA. Hatua hii inalenga kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana katika maeneo yote yenye umuhimu wa kimkakati kwa usalama, utalii na maendeleo ya Taifa. Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Mwasalyanda, amesema utekelezaji wa awamu hiyo mpya unafuatia mafanikio makubwa ya mradi wa awali wa minara 758, ambao umefikia zaidi ya asilimia 98 ya utekelezaji. Ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kumechangia kupunguza kwa kiasi kikubwa pengo la mawasiliano katika maeneo ya vijijini na pembezoni. Jumla ya vijiji 1,407 ambavyo awali havikuwa na mawasiliano, sasa vinafikishiwa huduma hiyo muhimu, hatua inayoboresha maisha ya wananchi na kuongeza fursa za kiuchumi. Aidha, Mhandisi Mwasalyanda ameongeza kuwa...

WAFCON QUALIFIERS 2026

Picha
23’ Tanzania 🇹🇿 1️⃣-0️⃣ 🇪🇹 Ethiopia  ⚽️Aisha Mnunka  @twigastars_ @caf_online