Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 22, 2026

MAJI TAKA YAKIDHIBITIWA AFYA BORA KWA KILA MWANANCHI

Picha

MAPATO MANISPAA YA TABORA YAPAA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora. HALMASHAURI ya manispaa Tabora imeendelea kupiga hatua kubwa kimaendeleo ikiwemo kufanikisha utekelezaji miradi ya maendeleo kutokana na kasi nzuri ya ukusanyaji mapato kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali. Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Dkt John Pima alipokuwa akiwasilisha mapendekezo ya rasimu ya bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 katika kikao cha Baraza la madiwani. Amefafanua kuwa kwa mwaka wa fedha 2026/2027 wanatarajia kukusanya zaidi ya sh bilioni 12 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali ikiwa ni sehemu ya rasimu ya mapendekezo ya bajeti yao kwa mwaka huu wa fedha. Amedokeza kuwa mapendekezo hayo ni ishara ya kazi nzuri ambayo imeendelea kufanywa na timu yake ya mapato kwa mwaka wa fedha uliopita ambapo walipanga kukusanya kiasi cha sh bilioni 8.6 na kupata mafanikio makubwa.  Dkt Pima amefafanua kuwa kati ya kiasi hicho sh bilioni 10.57 ni mapato halisi na kiasi cha sh bilioni 1.68 ni m...

JAB YAONYA WAAJIRI KATIKA VYOMBO VYA HABARI KUZINGATIA SHERIA KUEPUKA MIGOGORO YA KISHERIA

Picha
  Na Waandishi Wetu, Dodoma na Iringa. BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewasisitiza waajiri kwenye vyombo vya habari nchini kuzingatia kikamilifu masharti ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229, hususan wanapoajiri au kuwasainisha mikataba watumishi wa kada ya habari, ili kuepuka migogoro ya kisheria inayoweza kujitokeza baadaye. Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula tarehe 20-21 Januari, 2026 wakati wa ziara ya kikazi ya Bodi katika mikoa ya Dodoma na Iringa, ilipotembelea vyombo kadhaa vya habari kwa lengo la kukagua kiwango cha uzingatiaji wa Sheria hiyo kwa watumishi wanaojihusisha na shughuli za kihabari, wakiwemo wahariri, waandishi wa habari, watangazaji, wapiga picha waandaaji na waandishi wa kujitegemea. Akizungumza baada ya ziara hiyo, Wakili Kipangula amesema Bodi imebaini uwepo wa waandishi wenye sifa stahiki kwa mujibu wa Sheria kwenye vyombo hivyo, lakini bado hawajajisajili katika Mfumo wa TAI-HABARI ili kuomb...

WANAFUNZI WA USAGARA WAPATIWA ELIMU YA FEDHA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA TANGA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Tanga. WIZARA ya Fedha kupitia Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha imeendelea kutoa elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali ya jamii mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, jijini Tanga, kwa lengo la kuwajengea wananchi uelewa wa masuala ya kifedha na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi. Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu katika darasa la Elimu ya Fedha, Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Grace Muiyaza, alisema mafunzo hayo yanawalenga watumishi wa umma, wafanyabiashara wadogo, vikundi vya wajasiriamali, wananchi wa kawaida pamoja na wanafunzi kuanzia ngazi ya shule ya msingi, sekondari hadi vyuoni. “Tuko hapa tunatoa mafunzo kwa makundi yote ya jamii ya Tanga. Lengo letu ni kuwajengea uelewa wa masuala ya kifedha na kuwawezesha kushiriki vizuri katika shughuli za kiuchumi,” amesema Bi. Muiyaza. Ameeleza kuwa katika darasa la siku hiyo, walikutana ...

RAIS DKT.MWINYI AMUAPISHA AMINA MUUMINI KUWA NAIBU MKURUGENZI MKUU WA ZAECA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Ndg. Amina Muumini kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), kufuatia uteuzi wake uliofanywa hivi karibuni. Hafla ya uapisho huo imefanyika leo, tarehe 22 Januari 2026, Ikulu Zanzibar, sambamba na kikao cha Baraza la Mapinduzi.

WAZIRI MKUU MWIGULU AIPONGEZA SEKTA YA MADINI KWA KUONGEZA MAKUSANYO YA MAPATO

Picha
  Sekta ya Madini Tanzania imeingia kwenye kumbukumbu za Afrika, Nchi jirani zajifunza uendeshaji wa sekta ya madini Tanzania, Ataka kasi ya utafiti wa kina kuongezwa, Tume ya Madini yatakiwa kukomesha migogoro ya wachimbaji. Na Mwandishi Wetu, Dodoma. WAZIRI  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Sekta ya Madini kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika kuongeza makusanyo ya mapato ya Serikali na hivyo  kuiwezesha Tanzania kuandika historia mpya ya uendeshaji wa sekta hiyo Barani Afrika. Dkt. Mwigulu amesema mafanikio hayo yametokana na mageuzi makubwa ya kisera, kisheria na kiutendaji yaliyofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Madini, yaliyoiwezesha sekta hiyo kuwa jumuishi na shirikishi, huku Watanzania hususan vijana, wanawake na watu wenye mahitaji maalum wakishiriki kikamilifu katika mnyororo mzima wa thamani wa madini. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Januari 22, 2026, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo...

TANZANIA NA GATSBY ZAJADILI KUIMARISHA MABADILIKO YA KIUCHUMI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. SERIKALI na GATSBY Africa wamejadiliana vipaumbele vya Tanzania katika mabadiliko ya kiuchumi hasa katika kuimarisha ushindani wa uzalishaji wa viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050. Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa GATSBY Africa, Bw. Justin Highstead aliyeambatana na wajumbe wengine kutoka Taasisi hiyo. Alisema majadiliano hayo yanalenga vipaumbele vya nchi ambavyo vimeanishishwa katika Dira ya Taifa 2050 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5 na vinapaswa kutekelezwa ili kufikia lengo la taifa. “Hapa katikati katika utekelezaji Dira ya Taifa 2050 na Mpango wa Maendeleo, tumeangalia kwa pamoja, mageuzi ya kiuchumi kwanza ambapo ndani yake kuna ya mapinduzi ya viwanda, uwekezaji mkubwa wa kifedha pamoja na uwekezaji mkubwa wa kujenga rasilimali watu”, alisema Mhe. Balozi Omar. Aliongeza kuwa katika kikao hicho walijadiliana pia masu...