Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 25, 2026

RC MTANDA AAGIZA MPANGO WA KUPUNGUZA MADENI YA WAZABUNI NA WATUMISHI MAGU

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema Baraza la Madiwani linapaswa kufahamu madeni yote ya wazabuni na watumishi ili kuweka mpango wa kuyapunguza hatua kwa hatua katika miaka ijayo. Mhe. Mtanda ametoa kauli hiyo leo Juni 25, 2026, alipokuwa akizungumza katika Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani wa kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Amesema ni muhimu kutambua wazabuni wanaodaiwa pamoja na kiasi wanachodai ili halmashauri iweze kuandaa mkakati wa malipo utakaosaidia kupunguza madeni hayo ndani ya kipindi cha miaka miwili hadi mitatu. Aidha, ameeleza kuwa watumishi wanaoidai halmashauri wanapaswa kubainishwa pamoja na madai yao ili kuwepo mpango maalumu wa kulipa madeni hayo kwa awamu na hivyo kupunguza mzigo wa kifedha. Mkuu huyo wa Mkoa pia amesisitiza kuwa fedha zote za Serikali zinazodaiwa lazima zirejeshwe, akizitaka halmashauri zote za Mkoa huo kuunda timu maalumu (task force...