Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba 24, 2025

WAZIRI SHARIFF AZINDUA JENGO LA MRI HOSPITALI YA ABDULAA MZEE

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Pemba. WAZIRI wa Kazi na Uwekezaji Shariff Ali Shariff amesema Uwepo wa huduma ya MRI katika Hospitali ya Abdulaa Mzee Mkoani, Pemba ni hatua kubwa katika kuimarisha uwezo wa mfumo wetu wa afya na utawezesha wagonjwa kupata uchunguzi wa haraka, sahihi na wa uhakika.  Hayo ameyaeleza katika Hospitali ya Abdulla Mzee Mkoani wakati wa alipofungua jengo la huduma za MRI ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za Miaka 62 ya Mapinduzi Zanzibar.  Waziri Shariff amesema huduma ya MRI itaongeza uwezo wa madaktari kufanya maamuzi ya kitabibu kwa ufanisi zaidi, sambamba na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika sekta ya afya na itasaidia kupunguza kuchelewa kwa matibabu, kuokoa maisha na kupunguza gharama kwa familia na Serikali kwa ujumla.  Aidha amesema kuwa uwamuzi wa kuanzisha huduma ya MRI kisiwani Pemba unaonesha wazi dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Nane ya kusogeza huduma muhimu karibu kwa wananchi na kupunguza rufaa zisizo za lazima, kuimarisha ...

BANK YA AMANA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TRA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, leo tarehe 24.12.2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank ya Amana, Bw. Abubakar Athman Ali, katika ofisi za TRA jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili. Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo kuboresha mifumo ya ulipaji kodi kupitia taasisi za kifedha, pamoja na kuhamasisha walipakodi kulipa kodi kwa hiari kwa kutumia huduma za kibenki. Bw. Abubakar amesema Bank ya Amana ipo tayari kushirikiana kwa karibu na TRA katika kuhakikisha huduma bora zinapatikana kwa walipakodi, huku akiweka mkazo kwenye uboreshaji wa mifumo na elimu ya kodi kwa wateja wa benki hiyo. Kwa upande wake, Kamishna Mkuu Bw. Mwenda amepongeza ushirikiano huo na kusema kuwa hatua kama hizo zinaimarisha mazingira ya ulipaji kodi na kuchangia katika kukuza mapato ya Taifa.

DKT PIMA AAGIZA WAKUU WA SHULE KUSIMAMIA NIDHAMU

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora WALIMU Wakuu wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Manispaa Tabora wameagizwa kusimamia ipasavyo nidhamu za walimu na wanafunzi katika shule zao ili kuinua juu taaluma.   Agizo hilo limetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa hiyo Dkt John Pima alipokuwa akifunga semina maalumu ya Maafisa Elimu, Walimu wa Nidhamu, Waratibu na Wakuu wa shule zote mjini hapa. Amesema kuwa serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya maboresho makubwa ya miundombinu katika shule zote za Manispaa hiyo hivyo kuboreshwa mazingira ya ufundishaji na kujifunza. ‘Mazingira bora yaliyopo katika shule zetu ni chachu muhimu ya kuwezesha watoto wetu kufanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya kitaifa hivyo kuongeza ufaulu katika manispaa yetu, katika hili ni lazima tuimarishe nidhamu’, ameeleza. Dkt.Pima ameahidi kutoa motisha nzuri kwa kila mwalimu ambaye somo lake litapata alama A za ufaulu kwa idadi yoy...

HABARI PICHA

Picha
Shirika lisilo la kiserikali la Marafiki wa Serengeti Uswiss, wametoa msaada wa vifaa vya doria vya aina mbalimbali ikiwemo mahema, tochi, sleeping bags na matairi kwaajili ya kusaidia shughuli za doria. #wildanimals #travelphoto #wizarayamaliasilinautalii

USINDI AMCOS WANUNUA TREKTA KWA KILIMO NA KUJIONGEZEA KIPATO

Picha
  Na Lubango Mleka, Kaliua. CHAMA Cha Msingi Usindi AMCOS Ltd cha Kaliua Mkoani Tabora kimenunua Trekta kwa ajili ya kufanyia shughuli za Kilimo na pia watakodishia kufanyia shughuli za Kiuchumi kujiongezea kipato. Uzinduzi wa Trekta umefanywa Desemba 23, 2025 na Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Sosthenes Chakupanyuka, katika Mkutano Mkuu wa kufunga mwaka wa Chama hicho. Sosthenes amewapongeza kwa hatua hiyo kubwa na kusema Usindi AMCOS ni chama cha mfano wa kuigwa kwa Kaliua kwa kutimiza vyema lengo lao la kununua Trekta yao ya pili.Ameahidi kuwa nao pamoja  penye changamoto ashirikishwe. Pia amefurahishwa sana na namna ambayo wamekuwa wakijali jamii kwani wameweza kutoa mifuko 100 ya Simenti kwa ajili ya kujenga shule, kuweka umeme kwenye shule za Msingi na kujenga barabara ya kuelekea Zahanati ya Usindi. Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora Venance Msafiri ameahidi kuwapeleka wakulima mafunzo kuongeza Elimu ya Kilimo na Madereva wa Matrekta kuongeza ujuzi....