Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 19, 2026

BODI YA MAJI BONDE LA ZIWA TANGANYIKA YABORESHA VYANZO VYA MAJI

Picha
  Na Allan Kitwe, Kigoma.  BODI ya Maji ya Bonde laZiwa Tanganyika imefanikiwa kuboresha uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji vilivyopo katika Mikoa 8 na Halmashauri 28 za Miji, Manispaa na Wilaya zilizopo katika Ukanda wa Magharibi mwa Tanzania. Hayo yamebainishwa juzi na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Tanganyika Bona Mremi alipokuwa akiongea na wanahabari Ofisini kwake Mkoani Kigoma. Amefafanua shughuli zilizofanywa na Bodi hiyo katika Kanda hiyo kuwa ni kulinda, kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji ikiwemo mabwawa, mito, chemichemi, maziwa, maeneo oevu na fukwe za bahari. Shughuli nyingine ni kufuatilia mwenendo wa maji katika vyanzo vyote na kugawa maji kwa matumizi mbalimbali, kuongeza idadi ya Jumuiya za Watumiaji Maji kutoka 8 hadi 12 na kupanda miti zaidi ya milioni 2 katika vyanzo vya maji. ‘Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizotuwezesha kutekeleza majukumu yetu ya kusimamia, ...

KATIBU CCM SIMANJIRO ALETA FARAJA LOIBORSIRET

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro.  KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Wambura Igembya ameagiza bibi kizee mwenye umri wa miaka 105, Maria Nongululu mkazi wa kijiji cha Loiborsiret, kurerejeshewa ekari nne za shamba lake alilonyang'anywa na uongozi wa kijiji hicho. Katibu Wambura ametoa agizo hilo akiwa na sekretarieti ya CCM Wilaya hiyo, Katibu Mwenezi Mosses Makeseni, Katibu wa Wazazi Sasi Mirumbe na Katibu wa UWT Tichomo Sangija, katika ziara ya kuwashukuru kwa kuichagua CCM, kusikiliza kero na kukagua uhai wa chama. Katibu Wambura akizungumza Kwenye mkutano wa kijiji cha Loiborsiret ametoa agizo la bibi kizee huyo arejeshwe eneo lake kwani ni haki yake. ""Natoa maelekezo nikiwa katibu wa chama, udhibitisho wa eneo lake unajionyesha dhahiri, mama akarudishiwe eneo lake, kuwatumikia wananchi tuache kuwanyanyasa watu, tumechaguliwa ili tuwatumikie," amesema Igembya. Amesema CCM Wilaya ya Simanjiro, walipokea malalamiko na kero juu y...