SERIKALI YAZINDUA MFUMO "ONGEA NA WAZIRI, MWANACHI KUPEWA SAUTI YA MOJA KWA MOJA SEKTA YA AFYA
Na WAF, Arusha. SERIKAL imetangaza mwanzo wa enzi mpya ya uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi katika sekta ya afya baada ya kuzindua rasmi kwa mfumo wa kidijitali wa “Ongea na Waziri wa Afya” unaomuwezesha mwananchi kuwasiliana moja kwa moja na Wizara ya Afya saa 24 kwa siku. Hayo yamesemwa na Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Januari 26,2026 jijini Arusha. Waziri wa Afya, Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa, amesema mfumo huo ni utekelezaji wa vitendo wa dhamira ya Serikali ya kuisogeza huduma ya afya karibu na mwananchi na kuhakikisha sauti ya wananchi inatumika kama dira ya maboresho ya huduma. “Mfumo wa "Ongea na Waziri wa Afya" unatuma ujumbe ulio wazi kuwa sauti ya mwananchi si ya pembeni, bali ndiyo msingi wa maamuzi ya Serikali katika kuboresha huduma za afya,” amesema Waziri Mchengerwa. Amefafanua kuwa uzinduzi wa mfumo huo ni mapinduzi makubwa katika sekta ya afya kwa kuwa unajenga utamaduni mpya wa uongozi unaosiki...