URAMBO WAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI
Na Allan Kitwe, Urambo. HALMASHAURI ya Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora imefungua milango kwa wawekezaji wa ndani na nje kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali, kwa kuanzia wametenga eneo la ardhi lenye ukubwa wa hekari 72 kwa ajili ya kazi hiyo. Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Grace Quintine alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya halmashauri katika kikao cha baraza la madiwani. Amesema kuwa halmashauri hiyo ni miongoni mwa halmashauri zenye mazingira bora ya uwekezaji na ardhi nzuri inayofaa kwa shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara. Amedokeza kuwa maboresho makubwa ya miundombinu ya huduma za kijamii ambayo yameendelea kufanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kivutio muhimu kwa wawekezaji. Guintine amefafanua kuwa Urambo ni mahali salama kwa uwekezaji na kwa mwaka huu wa fedha wameratibu maeneo maalumu yanayofaa kwa uwekezaji na kutenga eneo lenye ukubwa w...