WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUZINGATIA KINGA NA TAHADHARI YA MAJANGA YA MOTO

 



Na Mwandishi Wetu, Morogoro.

WATUMISHI wa umma wametakiwa kutumia kikamilifu maarifa wanayoyapata katika kusimamia na kutekeleza kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto katika majengo na miradi yote ya serikali

Wito huo umetolewa na  Dkt. James Henry Kilabuko akizungumza kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Wenye Ulemavu) wakati wa semina ya usimamizi wa kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto iliyowakutanisha Wakurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Taasisi za umma 

Amesema changamoto ya ukosefu wa fedha kwa ajili ya ununuzi na ukarabati wa miundombinu ya kujikinga dhidi ya moto haipaswi kuwa kikwazo kwa watumishi wa umma kusubiri bila kuchukua hatua, bali watumie ipasavyo fursa na rasilimali zilizopo kujilinda wao wenyewe pamoja na kulinda mali za serikali.

Ameongeza kuwa maandalizi, tahadhari na ufuatiliaji wa mara kwa mara ni nguzo muhimu katika kupunguza athari zinazotokana na majanga ya moto, akisisitiza kuwa kinga ni bora kuliko tiba.










Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.