Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 27, 2026

BABA AMICHINJA MTOTO WAKE MCHANGA

Picha
  Na Allan Kitwe, Igunga MWANAUME mmoja mkazi wa Kijiji cha Imalanguzu, Kata ya Mwamakona, Tarafa ya Igurubi, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora amemchinja mtoto wake mchanga aliyekuwa na umri wa miezi miwili na kumjeruhi vibaya mke wake. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa , Richard Abwao ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Machi 25 mwaka huu majira ya saa 3 usiku huko katika Kitongoji cha Ibindo, kijiji cha Imalanguzu. Amebainisha kuwa mwanaume aitwaye Bunzali Jidola (30) Msukuma, mkulima, mkazi wa Imalanguzu alimchinja kwa kutumia kitu chenye ncha kali mtoto wake aitwaye Dorcas Bunzali aliyekuwa na umri wa miezi miwili. Ameongeza kuwa baada ya mauaji hayo alimjeruhi pia mke wake aitwaye Jeni Ndaki (24) Msukuma, mkulima, mkazi wa Kijiji cha Ibutamisuzi kwa kutumia kifaa hicho chenye ncha kali na kisha kutokomea kusiko julikana. Amesema majeruhi huyo aliokolewa na wasamaria wema na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga iliyoko Wilayani humo ...

WAKULIMA TABORA WANUFAIKA NA MNADA WA KWANZA WA KOROSHO

Picha
  Na Lubango Mleka, Tabora.  WAKULIMA wa zao la korosho mkoani Tabora wameanza kunufaika na fursa ya soko baada ya kuanza kwa mnada wa kwanza wa zao hilo, ambapo zaidi ya kilo elfu kumi na tatu zimeuzwa katika siku ya ufunguzi. Mafanikio hayo yameelezwa kuwa ni ishara ya kukua kwa zao la korosho mkoani humo, huku matarajio ya awali yakiwa ni kuuza kilo elfu kumi pekee. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Shabani Katalambula, amesema mwitikio wa wakulima ni mkubwa na unaonyesha wazi kuwa zao hilo linaweza kuwa tegemeo jipya la kiuchumi kwa wakazi wa Tabora. Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa kampuni ya Mateak Holdings Ltd, Violet Mordichai, amesema wamejikita katika kuwajengea uwezo wakulima kupitia elimu ya kilimo bora cha korosho, akisisitiza matumizi ya pembejeo ili kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao. Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora , Bi Upendo Wella, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, amewataka wakulima kujiunga na vyama vya ushirika ili kuwa na nguvu ya pamo...

VIJANA ZAIDI YA 60 WALIOHITIMU FDC NZEGA WAPATA AJIRA

Picha
  Na Allan Kitwe, Nzega.  TAASISI, Mashirika ya Umma na makampuni binafsi yamepongezwa kwa kutoa fursa za ajira kwa vijana wa kike na kiume wanaohitimu mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali kwenye Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) . Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Nzega (Nzega FDC) Nichodemus Shirima alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliomtembelea Ofisini kwake jana ili kujionea maendeleo ya chuo hicho. Ameshukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuvifanyia maboresho makubwa vyuo vyote vya maendeleo ya wananchi nchini na kuvipatia vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia hali ambayo imechochea vyuo hivyo kutoa elimu bora. ‘Zaidi ya vijana sitini (60) waliohitimu fani mbalimbali katika chuo chetu hapa Nzega wamepata ajira rasmi katika taasisi mbalimbali za umma na makampuni ya watu binafsi na wengine wamejiajiri na wanapata kipato cha uhakika’, ameeleza. Shirima amefafanua vijana walioajiriwa kuwa ni wa fani za ufundi bomba (zaidi...