Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 10, 2026

NDUGU WASHIKILIWA KWA KUMUUA SHEMEJI YAO 'KISA MGOGORO WA MASHAMBA'

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mbeya.  JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia ndugu wa familia moja ambao ni Solomon Mwambyale (68) na watoto wake wawili, Stephano Mwaisango (32) na Emmanuel Mwaisango (36), kwa tuhuma za mauaji ya Jenti Segelela (87) ambaye alikuwa shemeji yake na mtuhumiwa Solomon, wakidaiwa kumkata na kitu chenye ncha kali kisogoni na kisha kukimbia, chanzo kikiwa ni mgogoro wa mashamba ya ukoo na tamaa ya kujipatia mali kwa njia isiyo halali. Katika tukio la Pili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amesema wanamshikilia Bw. Charles Oden Mwakasege (32) fundi simu Mkazi wa Meta Jijini Mbeya na Bw. Isack Charles 'Bebwa' mkazi wa Shewa, kwa tuhuma za kuingilia mfumo wa kibiashara wa makampuni ya ukopeshaji wa simu. Kulingana na Kamanda Kuzaga katika taarifa yake ya leo Jumanne Februari 10, 2026 kwa Vyombo vya habari, watuhumiwa hao walikamatwa katika msako uliofanyika kuanzia Januari 27, 2026 katika maeneo mba...

WAZIRI WA FEDHA AWAHAKIKISHIA USHIRIANO WAWEKEZAJI NCHINI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WAZIRI wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewaahidi wawekezaji kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya uwekezaji nchini kwa manufaa ya pande zote mbili kutokana na manufaa ya sekta hiyo kwa uchumi wa nchi na wawekezaji. Mhe. Balozi Omar amesema hayo mjini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni mpya ya Uchimbaji Dhahabu Nyanzaga (Nyanzaga Mining Company Ltd), unaojengwa katika eneo la Nyanzaga Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza ambao hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 523. Alisema kuwa mradi huo ni mkubwa kujengwa Tanzania toka miaka zaidi ya 18 iliyopita ambapo mgodi wa Buzwagi ulijengwa. Na fursa zitaendelea hivyo kwa ukubwa wake. Lakini pia kuchangia uchumi wa nchi Kupitia kodi mbalimbali. “Ni mara yangu ya kwanza kukutana na uongozi wa mgodi wa dhahabu wa Nyanzagi na tumejadili kuhusu changamoto ya msamaha wa kodi na nimewaahidi kuwa hadi mwisho w...

NZUWASA YAONGEZA UZALISHAJI MAJI NZEGA

Picha
  Na Allan Kitwe, Nzega.  MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Nzega (NZUWASA) imeongeza mtandao wa upatikanaji huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Mji wa Nzega hadi kufikia kilomita 738.3 ambazo ni sawa na asilimia 99.5 ya eneo lote. Akizungumza na gazeti hili jana Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi Humphrey Mwiyombela amesema kuwa takribani eneo lote la Mji wa wa Nzega kwa sasa limefikiwa na huduma ya maji safi na salama. Amebainisha kuwa mafanikio hayo yametokana na mikakati yao ya kuendelea kuzalisha maji kupitia vyanzo vyake vya ndani kwa lengo la kupanua wigo wa upatikanaji huduma hiyo katika maeneo yote ya Mji huo na maeneo jirani. Ametaja mkakati mwingine uliosaidia kuimarisha upatikanaji huduma hiyo kuwa ni kuendelea kushirikiana na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama na Shinyanga (KASHWASA). Mkurugenzi amedokeza kuwa mahitaji ya maji kwa wakazi wa Mji huo kwa siku ni mita za ujazo 5,600 na kiasi kinachozalishwa kupitia vyanzo vya...

SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA AFUA ZA KINGA DHIDI YA VVU, MAGONJWA YA NGONO NA HOMA YA INI

Picha
  Na WAF, Morogoro.  SERIKALI imeendelea na utekelezaji wa afua za kinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU), Magonjwa ya Ngono (STIs) na Homa ya Ini  kwa ngazi ya mikoa na jamii, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufikia malengo ya kitaifa ya kudhibiti maambukizi mapya na kulinda afya ya mwananchi. Hayo yamebainishwa Februari 10, 2026 na Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini (NASHCoP) Dkt. Prosper Faustine wakati wa ufunguzi wa mkutano wa waratibu wa afua za UKIMWI nchini, kinachoendelea mkoani Morogoro mkutano ambao unaangazia kufanya mapitio ya utendaji na utekelezaji wa huduma mbalimbali za kinga. "Upimaji wa VVU, matumizi ya dawa kinga za PrEP, tohara ya hiari ya wanaume, programu za kondomu pamoja na afua zinazolenga wasichana balehe na wanawake vijana na wavulana balehe na wanaume vijana zimekua endelevu ili kufikia lengo la 95 95 95 ifikapo mwaka 2030" amesema Dkt. Faustine. Mapitio hayo yanalenga kubaini mafanikio yali...

TASAC YATOA ELIMU YA USAFIRI MAJINI FUKWE YA MSIMBATI - MTWARA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mtwara.  SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa elimu ya usafiri kwa njia ya maji kwa wadau wake katika fukwe ya Msimbati, mkoani Mtwara.  Elimu hiyo imelenga kuongeza uelewa kuhusu matumizi salama ya vyombo vya usafiri majini, ikiwemo kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama wakati wa safari. Katika utoaji wa elimu hiyo, maafisa wa TASAC wamewakumbusha wamiliki na waendeshaji wa vyombo vya usafiri majini, wavuvi pamoja na abiria umuhimu wa kuvaa vifaa vya kujikinga kama vile jaketi za kuokoa Maisha (life jacket), kufanya ukaguzi wa vyombo kabla ya safari na kuepuka kupakia abiria au mizigo kupita kiasi.  Wadau walioshiriki wamepongeza juhudi za TASAC kwa kuendelea kuwafikia moja kwa moja katika maeneo yao ya kazi na kutoa elimu yenye tija. Wamesema elimu hiyo itasaidia kupunguza ajali za majini na kuongeza usalama wa vyombo na watumiaji wake, huku wakiahidi kushirikiana na TASAC katika kutekeleza miongozo ya usalama kwa manu...

JESHI LA POLISI KUENDELEA KUWEKA JITIHADA ZA KUNUNUA MBWA WAPYA WA KISASA WENYE UWEZO WA KUBAINI,KUZUIA NA KUMDHOOFISHA MHALIFU.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.  MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, amesema Jeshi la Polisi litaendelea kuweka jitihada mbalimbali za kununua mbwa wapya wa kisasa na wenye uwezo ili kuboresha muonekano wa mbwa wa Polisi mwenye umbo lenye kumdhoofisha mhalifu. IGP Wambura, ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Kikosi cha Mbwa na farasi wa Mikoa na Wataalam Waongoza Mbwa na Farasi kikao kilichofanyika jijini Dar es salaam Februari 9,2026 huku akiweka msisitizo kwenye eneo la utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwatumia Wanyama kazi katika kudhibiti uhalifu kwenye maeneo yao. Akizungumza na Watendaji hao IGP Wambura, amebainisha kuwa, Kikosi hicho kina umuhimu mkubwa kiusalama kwa kuwa Doria za mipakani na maeneo mengine muhimu hulazimika kutumia mbwa na farasi kwani ni rahisi kupenya kwenye maeneo ambayo gari haliwezi kupita kwa urahisi. Amesema, Jeshi la Polisi lina Mbwa na Farasi wanaofanya kazi katika bandari, viwanja vya ndege n...

RC SENYAMULE AUKARIBISHA UMIKIDO, AITAKA KUWA CHACHU YA MAWASILIANO KATI YA SERIKALI NA WANANCHI

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, ameukaribisha Umoja wa Vyombo vya Habari vya Mitandao ya Kijamii Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO) na kuutaka kuwa chachu ya kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi kupitia utoaji sahihi wa taarifa pamoja na ubunifu wa maudhui. RC Senyamule ametoa kauli hiyo leo Februari 9, 2026, mara baada ya viongozi wa UMIKIDO kufika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha na kuomba ushirikiano na Serikali ya Mkoa wa Dodoma. “Hongereni kwa kuanzisha umoja huu. Nimefurahishwa sana kwani utarahisisha kazi na kuwa kiunganishi muhimu kati ya Serikali ya Mkoa na vyombo vya habari vya mitandaoni. Tulitamani kupata watu wanaozungumza lugha moja na Serikali, na tunaamini ninyi ni wazalendo,” amesema Mhe. Senyamule. Ameeleza kuwa uwepo wa umoja huo utaisaidia Serikali kufikisha taarifa kwa wananchi kwa ufanisi zaidi, sambamba na kuongeza uelewa wa umma kuhusu shughuli na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ...