VIONGOZI WA DINI SINGIDA NA DODOMA WAHIMIZA VIJANA KULINDA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Na Hamida Ramadhan, Dodoma. VIONGOZI wa Dini kutoka mikoa ya Singida na Dodoma wamewataka vijana kuepuka vishawishi vya vurugu na mifarakano ya kisiasa, wakisisitiza kuwa kulinda amani ni jukumu la kila Mtanzania kadri Taifa linavyoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo. Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma katika kongamano la viongozi wa dini mbalimbali kutoka Kanda ya Kati, lililolenga kuliombea Taifa amani na utulivu kuelekea uchaguzi huo. Akizungumza katika kongamano hilo, Askofu Evance Chande wa Kanisa la Carmel Assemblies of God amesema vijana wanapaswa kutumia nguvu zao katika kujenga Taifa badala ya kushiriki katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa nchi. “Tunapaswa kuikumbatia amani kama tunavyokumbatia imani zetu. Uchaguzi ukipita, Tanzania inabaki kuwa moja. Tusikubali kugawanywa kwa misingi ya kisiasa,” amesema Askofu Chande. Kwa upande wake, Sheikh Mustapha Rajab, Sheikh wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ...