Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 26, 2026

TANZANIA YAIMARISHA TAHADHARI DHIDI YA MLIPUKO WA EBOLA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  NAIBI Waziri wa Afya Mheshimiwa. Dkt. Florence Samizi amesema Tanzania imeendelea na hatua za kuzuia na kuimarisha utayari dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo unaoendelea katika nchi za Jamhuri ya Demokrasia Kongo na Uganda, huku akisisitiza mshikamano wa kikanda na umuhimu wa ushirikiano wa pamoja katika kulinda usalama wa afya wa wananchi. Dkt. Samizi amesema hayo leo Mei 26, 2026 kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa mjadala kuhusu mlipuko wa Ebola katika nchi hizo, ulioandaliwa jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, ambapo ameshiriki kwa njia ya mtandao akiwa katika ofisi za Wizara jijini Dodoma. Katika mjadala huo, Tanzania imeeleza mshikamano wake na Serikali pamoja na wananchi wa DRC na Uganda kufuatia mlipuko huo, huku ikitoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao pamoja na wahudumu wa afya waliopo mstari wa mbele wakitoa huduma. Aidha Dkt. Samizi amesema Tanzania inatambu...

JMAT: TANZANIA HAINA UBAGUZI WA KIDINI

Picha
  Na Lubango Mleka, Dodoma.  KATIBU wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Askofu Israel Maasa, amesema kwa zaidi ya nusu karne Watanzania wa dini zote wamekuwa wakiishi kwa upendo, mshikamano na kuheshimiana bila kujali tofauti zao za kiimani. Askofu Maasa amesema Tanzania imeendelea kuwa mfano wa amani, umoja na uhuru wa kuabudu kwa dini zote bila ubaguzi wowote, hali iliyosaidia kudumisha mshikamano wa kitaifa kwa miaka mingi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, alisema jumuiya hiyo imesikitishwa na taarifa zilizotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania zinazodai kuwepo kwa ubaguzi wa kidini nchini. Alisema taarifa hizo, ambazo zinadaiwa kuungwa mkono na baadhi ya wabunge pamoja na Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Marekani, haziakisi hali halisi ya Tanzania na zimewasikitisha pamoja na kuwafedhehesha wananchi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa JMAT, Alihadi Mussa Salum, amesema hakuna kundi lolote nchini linalonyimwa uhuru wa kuabudu au kuumizw...