Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 19, 2025

MZIZE ASHINDA TUZO YA MFUNGAJI BAO BORA LA MWAKA 2025 YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU AFRIKA.

Picha
MSHAMBULIAJI  wa Yanga, Clement Mzize, ameshinda tuzo ya Mfungaji wa Bao Bora la Mwaka 2025 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Mzize ametangazwa mshindi wa kipengele hicho katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo inayoendelea kufanyika Rabat, Morocco, leo Jumatano, Novemba 19, 2025. Bao lililompa tuzo hiyo ni lile alilofunga dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024/2025, uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Januari 4, 2025, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1. Mzize ameibuka mshindi mbele ya Ghizlane Chebbak, Abdellah Ouazane, Barbra Banda, Anas Roshdy, Asharaf Tapsoba, Calvin Fely, Ibrahim Adel, Jean Claude, Ndabayithethwa Ndlonolo, Refiloe Jane, Oussama Lamlioui na Soufiane Bayazid.

TIMU YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAMTEMBELEA MDAU WA UTALII MZEE GEOFF FOX.

Picha
Na Lubango Mleka, Iringa. TIMU  ya Wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi, Bi. Dainess Kunzugala leo Novemba 19,2025 imemtembelea mdau mkubwa  wa utalii na uhifadhi  kwa Kanda za Nyanda za juu Kusini Mzee Geoff Fox wilayani Mufindi mkoani Iringa lengo ikiwa ni kumhamasisha kuingia katika kuwania tuzo za uhifadhi na utalii za Serengeti 2025. Mzee Fox anamiliki kambi za kitalii (lodges) 7 ndani ya hifadhi na ndiye mwanzilishi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani. Aidha, Mzee Fox ni mwekezaji wa kwanza wa kambi ya utalii katika Hifadhi ya Taifa Ruaha na ni kinara katika uhifadhi kwa kutunza na kulinda miti ya asili.

MRADI WA MAJIKO BANIFU WATAMBULISHWA HANANG

Picha
Majiko banifu 1,583 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku, Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku TZS 11,200. Na Mwandishi Wetu, Hanang. WAKAZI wa Hanang waaswa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi na salama ya kupikia. Rai hiyo imetolewa  leo tarehe 19 Novemba, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mheshimiwa Almishi Hazali wakati wa uzinduzi wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku. "Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia katika kutunza na kuhifadhi mazingira" alisema Mhe. Hazali. Mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni mwendelezo wa  juhudi za serikali  katika kutunza mazingira na kuboresha afya za  wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia. Aidha Serikali imeweke ruzuku ya asilimia 80 katika  kila j...

TUMEKUJA KUTIMIZA NDOTO YA RAIS SAMIA YA KULIJENGA TAIFA- MHE. CHANDE

Picha
Na Mwandishi wetu – Dodoma NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Hamad Chande (Mb) ameitaka menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa ushirikiano katika kutimiza ndoto za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulijenga Taifa. Ameyasema hayo katika kikao na menejimenti ya Wizara hiyo kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma Novemba 18,2025 mara baada ya kuripoti ofisini hapo. “Rais Samia amesema miradi tunayoihitaji kutekeleza ni mingi muda ni mchache na ndani ya siku 100 yako mambo anayotaka tuwe tumeyafikia hivyo sisi hatuwezi kuyafikia bila uwepo  wenu ninyi kwa taaluma zenu na mashirikiano yenu ya dhati kwetu” amesema Mhe. Chande. Pia ameitaka menejimenti hiyo kutekeleza falsafa ya  “Ishi vyema na watu ,Ufanye kazi kwa utu, Uwatambue watu ili na wewe uwe mtu mbele za watu."

MC PILIPILI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHAMBULIWA, POLISI DODOMA WACHUNGUZA CHANZO

Picha
Na Jasmine Shamwepu, Dodoma. JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma limethibitisha kifo cha msanii maarufu wa vichekesho Emmanuel Mathias Matebe, maarufu kama MC Pilipili, kilichotokea Novemba 16, 2025 katika Kituo cha Afya Ilazo, jijini Dodoma, ambako alikuwa akipatiwa matibabu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Novemba 19, 2025, Kamishna Msaidizi wa Polisi William Mwamafupa alisema kuwa MC Pilipili alifikishwa kituoni hapo akiwa katika hali mbaya na alifariki dunia majira ya saa 9:00 alasiri. Kwa mujibu wa taarifa za awali, kabla ya kifo chake, majira ya saa 8:00 mchana, msaidizi wake Hassan Ismail alipigiwa simu na mtu asiyefahamika na kuitwa mahali fulani kwa mazungumzo.  Baada ya muda, walitokea watu watatu ambao hawakufahamika wakimtumia MC Pilipili wakiwa ndani ya gari dogo jeupe na kumkabidhi kwa msaidizi wake kisha kuondoka kwa haraka. Wataalamu wa afya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamebaini kuwa marehemu alionyesha dalili za kushambuliwa sehemu mbalimba...

RAIS DKT.SAMIA AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU CHAMWINO

Picha
 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao Kazi cha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kilichofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 19 Novemba, 2025.

CHAMA CHA MAPINDUZI KUWASHUGHULIKIA WATENDAJI WAZEMBE

Picha
Na Jasmine Shamwepu, Dodoma. CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa kitachukua hatua kali dhidi ya viongozi wote wazembe na wanaojihusisha na vitendo vya rushwa, kikisisitiza kwamba hakitavumilia kiongozi yeyote anayeshindwa kuwajibika kwa wananchi.  Akitoa kauli hiyo jijini Dodoma, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi, amesema chama kitaweka vipimo maalum vya kupima utendaji wa viongozi katika ngazi zote ili kuhakikisha uwajibikaji unazingatiwa kikamilifu. "Mawaziri na Manaibu Mawaziri walioteuliwa na Rais wanapaswa kwenda sambamba na kasi ya utendaji ya kiongozi wa nchi, akibainisha kuwa ingawa baadhi yao ni wapya na wanafurahia uteuzi, wanapaswa kufahamu kuwa Rais anataka kazi yenye matokeo kwa wananchi na hana mzaha katika masuala ya utumishi wa umma." Amesisitiza kuwa CCM haitasita kumchukulia hatua yoyote atakayekwenda kinyume na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan. Aidha, Kihongosi amesema chama kipo bega kwa bega na ...