MZIZE ASHINDA TUZO YA MFUNGAJI BAO BORA LA MWAKA 2025 YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU AFRIKA.












MSHAMBULIAJI  wa Yanga, Clement Mzize, ameshinda tuzo ya Mfungaji wa Bao Bora la Mwaka 2025 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Mzize ametangazwa mshindi wa kipengele hicho katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo inayoendelea kufanyika Rabat, Morocco, leo Jumatano, Novemba 19, 2025.

Bao lililompa tuzo hiyo ni lile alilofunga dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024/2025, uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Januari 4, 2025, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Mzize ameibuka mshindi mbele ya Ghizlane Chebbak, Abdellah Ouazane, Barbra Banda, Anas Roshdy, Asharaf Tapsoba, Calvin Fely, Ibrahim Adel, Jean Claude, Ndabayithethwa Ndlonolo, Refiloe Jane, Oussama Lamlioui na Soufiane Bayazid.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.