Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 4, 2026

MJOMBA MATATANI KWA KUMPIGA NA KUMNING'INIZA MTOTO DIRISHAJI KWA KUUNGUZA MBOGA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  JESHI la Polisi nchini Tanzania linamshikilia Joseph Mbalamwezi Francis Mkazi wa Mtaa wa Imalamakoe B, Wilayani Urambo, Mkoani Tabora kwa tuhuma za kumfanyia mtoto ukatili wa kufungwa kamba miguuni na mikononi na kisha kumning'iniza dirishani. Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime ameviambia Vyombo vya habari leo Jumatano  Machi 04, 2026 kuwa tukio hilo lilitokea Machi 02, 2026 na mtoto aliyekuwa anafanyiwa ukatili huo ana umri wa miaka 10 na kwamba mtuhumiwa ni Mjomba wake ambaye walikuwa wakiishi pamoja. "Sababu za kumfanyia ukatili huo wa kupigwa na kisha kuning'inizwa inadaiwa ni baada ya mtoto huyo kuunguza mboga (nyama) aliyokuwa anapika." Amesema Kamanda Misime. Jeshi la Polisi pia limewashukuru waliotoa taarifa za tukio hilo na kufanikisha mtoto huyo kuokolewa na kwenda kupatiwa matibabu na mtuhumiwa kukamatwa, Polisi ikisisitiza ushirikiano zaidi katika kuwalinda na kuzuia vitendo vya ukatili...

MHE MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA MARA AGNESS MARWA AGAWA VIFAA VYA SALOON.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mara.  KATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha vijana,Mbunge wa viti maalumu mkoa wa mara Mhe, Agness Marwa amegawa vitendea kazi vya saloon za kike na kiume Kwa vijana zaidi 30 katika manispaa ya Musoma mkoa wa Mara. Dhamira hiyo ni kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi na kuunga mkono serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo. Akizungumza katika kikao cha wajasiliamali  kilichofanyika Manispaa ya Musoma, Mbunge Agnes amesema ataendelea kuyafukia makundi mablimabli wakiwemo wajasiliamali Mali wote katika mkoa wa mara. Mhe. Agnes amesema azma hiyo ni kuunga mkono jitihada za mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan zinazojikita kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo katika kujikwamua kiuchumi. Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Manispaa ya Musoma Juma Chikoka amempongeza Mbunge huyo ambapo amewataka wajasiliamali hao kuvitumia vifaa hivyo Kwa Lengo lililokusudiwa ili kujiongezea kipato. Nao baadhi ya wajasiliamal...