Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 3, 2026

WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKI KUDHIBITI SILAHA

Picha
  Na. Hamida Ramadhan, Dar Es Salaam. MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura amewataka watanzania wote kushiriki katika jukumu la udhibiti na usimamizi wa Silaha ili kulinda nchi yetu ikiwa ni utekelezaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. IGP Wambura ameyasema hayo Februari 3, 2026 Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kamati ya Udhibiti na Usimamizi wa Silaha pamoja na kufungua Kikao cha kwanza cha Kamati hiyo kinachofanyika kwa siku tatu ambapo zitawasilishwa mada mbalimbali za  kuwajengea uwezo wana kamati ili kufahamu majukumu yao, sheria na kanuni,itifaki za kikanda na kimataifa zitakazo waongoza katika jukumu la kudhibiti na kusimamia silaha na risasi nchini. Amesema, changamoto ya uzagaaji wa silaha haramu kwa kiasi kikubwa ulitokana na migogoro kwa baadhi ya nchi zinazoizunguka Tanzania, kuwepo kwa mipaka isiyo rasmi na ukiukwaji wa sheria.  Aidha, alisema changamoto hiyo ilikuwa kubwa katika miaka ya 2000 kurudi nyuma kutokana na machaf...

SERIKALI YAPUNGUZA KIFAFA CHA USUBI KWA ASILIMIA 40

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imefanikiwa kupunguza kiwango cha ugonjwa wa kifafa kinachohusiana na ugonjwa wa usubi kutoka asilimia 60 hadi asilimia 40 ndani ya kipindi cha miaka sita. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, wakati wa kikao kazi cha tathmini ya tafiti za ugonjwa wa Kifafa kilichofanyika Februari 3, 2026 jijini Dar es Salaam, kikihusisha wilaya ya Mahenge mkoa wa Morogoro. Dkt. Shekalaghe amesema ugonjwa wa kifafa unaohusishwa na usubi umekuwa changamoto kubwa katika eneo la Mahenge kwa miaka mingi, lakini kupitia utekelezaji wa tafiti za kisayansi na utoaji wa dawa kwa jamii, serikali imefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi kwa zaidi ya asilimia 22 kwa eneo la Mahenge. Ameeleza kuwa serikali imekuwa ikiendesha zoezi la kutoa dawa ya Ivermectin kwa jamii yote kwa zaidi ya miaka 25, lengo likiwa ni kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa usubi, ambao unahusishwa na baadhi ya aina za kifafa katika maene...

MAJIKO BANIFU YA RUZUKU YAPIGA HODI SHINYANGA.

Picha
Majiko banifu 5,236 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Shinyanga, Wilaya nne (4) kunufaika na mradi. Na Lubango Mleka, Shinyanga. SERIKALI ya Mkoa wa Shinyanga kupitia Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Katibu tawala msaidizi rasilimali watu, Ndugu David Lyamongi leo Februari 03, 2026 imepokea mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku. Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa ya mradi, Mhandisi Mwandamizi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Deusdedit Malulu amesema, Serikali kupitia REA imekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku ambao utasaidia kupunguza athari za kiafya na mazingira zitokanazo na matumizi ya nishati  isiyo salama ya kupikia. Aidha, usambazaji na uuzaji wa majiko haya banifu ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia wenye dhima mpaka  ifikapo mwaka 2034 zaidi ya asilimia themanini 80% ya watanzania wawe wanatumia nishati safi y...

ZEC KUCHOMA NYARAKA ZOTE ZILIZOTUMIKA KATIKA UCHAGUZI MKUU 2025

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imeidhinisha rasmi zoezi la kuteketeza nyaraka zote zilizotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2025, baada ya kukamilika kwa muda wa siku 90 tangu kumalizika kwa uchaguzi huo. Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha Tume kilichofanyika tarehe 2 Februari, 2026, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kisheria kuhakikisha mchakato mzima wa uchaguzi unakamilika kwa uwazi, ufanisi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo Kwa mujibu wa ZEC, Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari makao makuu ya ZEC Maisara,Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mhe.Jaji George J. Kazi  alisema zoezi hilo linafanyika kwa kuzingatia kifungu cha 98(3) cha Sheria ya Uchaguzi namba 4 ya mwaka 2018, kinachoitaka Tume kuharibu nyaraka zote zinazohusiana na Uchaguzi Mkuu baada ya kupita siku 90 tangu kukamilika kwa uchaguzi husika. Mwenyekiti  ameeleza kuwa kabla ya kuidhinisha utekelezaji wa zoezi hilo, ilijiridhish...

WANANCHI SELELA WAISHUKURU GEF- UNDP KUKAMILISHA MRADI WA MAJI.

Picha
Na Mwandishi wetu, Monduli. WANANCHI wa kijiji cha Selela ,Kata ya Selela,wilaya ya Monduli, mkoa Arusha, wameshukuru Mfuko wa Mazingira Duniani(GEF)  kupitia programu ya ruzuku ndogo inayotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kwa kufanikisha  mradi wa maji kutoka katika chanzo cha maji cha  Kabambe  ambao umekuwa na manufaa makubwa. Mradi huo,  umetekelezwa na shirika la waandishi wa habari la kusaidia jamii za asili la  MAIPAC  ikiwa ni sehemu ya mradi wa Kuheshimu na Kulinda maarifa ya jamii za asili katika uhifadhi (Respecting and Preserving Indigenous Traditional Knowledge in Conservation) ambao pia umetekelezwa katika jamii wa Wahdzabe katika eneo la bonde la Eyasi wilaya ya Karatu. Wakizungumza  na waandishi wa habari waliotembelea mradi huo, Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Longidonyi Lunda  akiwa pamoja na viongozi wa kamati ya maji na mazingira ya kijiji hicho, amese...

WATUMISHI IGUNGA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Picha
Na Mwandidhi Wetu, Igunga. MKUU wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi amempongeza Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha maslahi ya Watumishi ikiwemo fedha za likizo. Hamisi ametoa wito huo, wakati wa kikao kazi na Watumishi wa kata ya Igunga, Bukoko na Mtungulu kilichofanyika katika ukumbi wa Father Albert Bolle mjini hapa. "Ni fahari  kwetu watumishi kwa sababu Mhe. Rais. Dk. Samia Suluhu Hassan katuletea fedha za likizo za kutosha na katuongezea mishahara ikiwemo kupandisha vyeo," amesema. Aidha, amewataka Watumishi hao, kuendelea kufanya kazi kwa weledi na wasione tabu kwa sababu waliomba kazi na wamepata kazi hivyo wasione kazi kufanya kazi.

MWILI ULIOKATIKA VIPANDE WAKUTWA KWENYE RELI, TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora. MWILI wa mwanaume ambaye hajafahamika jina lake umekutwa kwenye reli ya treni huku ukiwa umekatwa vipande katika Mtaa wa Kombomasai, Kata ya Malolo, Manispaa ya Tabora huku ikihisiwa kuwa umeburuzwa na treni iliyopita usiku. Akizungumzia tukio hilo jana diwani wa Kata hiyo Naomi Kasanga ameeleza kuwa akiwa nyumbani kwake saa 2 asubuhi alipigiwa simu na wananchi wakimjulisha kuwepo mwili huo kwenye reli ya treni ukiwa umekatika vipande. Ameeleza kuwa alipofika eneo la tukio alikuta mwili huo wa mwanaume ambao unadhaniwa kuwa umeburuzwa na treni iliyopita usiku wa kuamkia jana baada ya kugongwa ila haijafahamika ni nani na alikuwa anatokea wapi. ‘Baada ya kuona mwili huo nilitoa taarifa kituo cha polisi na askari walikuja mara moja eneo hilo na kuuchukua kwa ajili ya uchunguzi zaidi, nashukuru sana wananchi kwa ushirikiano wenu na kunipa taarifa mapema’, amesema. Mheshimiwa diwani ameomba Wataalamu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuweka alama ya hatari kat...

VIGOGO WAWILI CCM WAFARIKI DUNIA

Picha
 L Na Allan Kitwe, Tabora KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyewahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Mshauri wa Chama na Kiongozi katika nafasi mbalimbali za chama na serikali Mzee Nassoro Hamdan (84) amefariki dunia jana jijini DSM. Aidha aliyewahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Tabora kwa miaka 20, Bi.Munde Abadllah Tambwe naye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.   Akizungumzia misiba hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Saidi Nkumba ameeleza kusikitishwa na taarifa hizo na kubainisha kuwa wameondokewa na watu muhimu sana kwa chama na jamii kwa ujumla. Ameeleza kuwa Mzee Hamdani ambaye ni Mwanzilishi wa Kampuni ya Mabasi ya NBS Classic Ltd ya Mjini Tabora na Munde walikuwa nguzo muhimu sana kwa Chama kwa jinsi walivyokuwa wakijitoa, hakika chama kimepata pigo kubwa. Ameongeza kuwa Mzee Hamdan ambaye alijulikana zaidi kwa jina la NBS ametumikia chama hicho tangu akiwa kijana mdogo na aliendelea hiv...

MRADI WA MAJIKO BANIFU WATAMBULISHWA GEITA

Picha
Majiko banifu 11,022 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Geita, Wilaya tano (5) kunufaika na mradi Na Mwandishi Wetu, Geita. SERIKALI ya Mkoa wa Geita kupitia Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Geita ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Mipango na Uratibu, Ndugu Deodatus Kayango leo Februari 02, 2026 imepokea mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku. Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa ya mradi, Mhandisi Mwandamizi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Deusdedit Malulu amesema, Serikali kupitia REA imekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku ambao utasaidia kupunguza athari za kiafya na mazingira zitokanazo na matumizi ya nishati  isiyo salama ya kupikia. Aidha, usambazaji na uuzaji wa majiko haya banifu ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia wenye dhima mpaka  ifikapo mwaka 2034 zaidi ya asilimia themanini 80% ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupiki...

VYUO VIKUU NA HALMASHAURI KUSHIRIKIANA KATIKA MPANGO WA ARDHI

Picha
  Na Mwandishwi Wetu, Dodoma. SERIKALI imeelekeza wadau kuhakikisha uwekezaji unaofanyika karibu na kampasi mpya 16 za vyuo vikuu unazingatia mpangilio wa miji, usalama na viwango vya kitaifa ili kuzuia ujenzi holela na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi mahitaji ya wanafunzi, watumishi na jamii jirani. Akizungumza Februari 02, 2026 jijini Dodoma, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi,amesema kuwa halmashauri na serikali za mitaa zinapaswa kutenga ardhi na kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi kwa kushirikiana na vyuo husika. Prof. Mushi amesisitiza kuwa mipango hiyo lazima izingatie viwango vya kitaifa vya upangaji miji na kuondoa migongano ya matumizi ya ardhi. Profesa Mushi pia amevielekeza vyuo vikuu kufungua milango ya ushirikiano na sekta binafsi kupitia ubia rasmi (PPP) katika ujenzi wa hosteli, vituo vya biashara na miundombinu maalum. Amesema mashauriano ya mara kwa mara kati ya vyuo na serikali za mitaa ni muhimu ili kuoanish...

CSR YA CHUSA MINING LTD ILIVYO MIRERANI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani. KAMPUNI ya Chusa Mining LTD kupitia Mkurugenzi wake Joseph Mwakipesile, imefanikisha miradi mbalimbali ya kuwajibika kwa jamii (CSR) mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ikiwemo ujenzi wa wodi ya wanawake na watoto katika kituo cha afya Mirerani. Fundi msimamizi wa ujenzi wa wodi ya wanawake, watoto na ofisi katika kituo cha afya Mirerani, Abdalah Said anaeleza kuwa hatua iliyopo hivi sasa ni jengo hilo limefikia hatua ya lenta. "Mbao za kupanua zipo tayari kwa hiyo baada ya siku tatu upauzi utaanza kwani tunamalizia kufunga baraza kwa kumimina," amesema Abdallah. Katibu wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) Tawi la Mirerani Rachel Njau ametoa wito kwa wamiliki wa migodi na wachimbaji wa madini ya Tanzanite, kuipenda Mirerani na kuwezesha miradi ya CSR ili kurudisha kwa jamii pindi wanapozaliwa madini. Ameishukuru kampuni ya Chusa Mining LTD, kwa ujenzi wa wodi ya wanawake na watoto ambayo ipo kwenye hatua ya...