WATUMISHI IGUNGA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI
Na Mwandidhi Wetu, Igunga.
MKUU wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi amempongeza Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha maslahi ya Watumishi ikiwemo fedha za likizo.
Hamisi ametoa wito huo, wakati wa kikao kazi na Watumishi wa kata ya Igunga, Bukoko na Mtungulu kilichofanyika katika ukumbi wa Father Albert Bolle mjini hapa.
"Ni fahari kwetu watumishi kwa sababu Mhe. Rais. Dk. Samia Suluhu Hassan katuletea fedha za likizo za kutosha na katuongezea mishahara ikiwemo kupandisha vyeo," amesema.
Aidha, amewataka Watumishi hao, kuendelea kufanya kazi kwa weledi na wasione tabu kwa sababu waliomba kazi na wamepata kazi hivyo wasione kazi kufanya kazi.








Maoni