Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 25, 2026

RUVUMA YAPOKEA MAJIKO BANIFU 7,648 KWA BEI YA RUZUKU.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Songea- Ruvuma. MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, leo Mei 25, 2026 amepokea rasmi mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupitia kampuni ya Burn Manufacturing Company Limited. Mradi huo unalenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia usambazaji wa majiko banifu yenye teknolojia ya kisasa kwa gharama nafuu kutokana na ruzuku inayotolewa na Serikali. Akizungumza wakati wa kupokea mradi huo, Mkuu wa Mkoa ameipongeza REA kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati safi ya kupikia nchini, akieleza kuwa majiko banifu yana mchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi pamoja na kulinda mazingira. Amesema matumizi ya majiko hayo yatasaidia kupunguza athari zinazotokana na matumizi ya kuni na mkaa usio salama, ikiwemo moshi unaosababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji, hususan wanawake na watoto. Mheshi...