Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 1, 2025

DKT. MPANGO AZINDUA MAONESHO YA 32 NANENANE KITAIFA JIJINI DODOMA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amezindua rasmi Maonesho ya 32 ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni, jijini Dodoma yenye kauli mbiu isemayo "Chagua Viongozi bora kwa Maendeleo Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025". Dkt. Mpango amesema kuwa Tanzania inaadhimisha Maonesho ya 32 ya Nanenane yenye hadhi ya Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kukuza uchumi na kuchochea matumizi ya teknolojia bora na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa. Tangu asubuhi ya leo, maelfu ya wananchi kutoka mikoa mbalimbali wamejitokeza kutembelea banda ya Wizara ya Madini na Taasisi zake, wakipata elimu juu ya mchango wa sekta ya madini katika kuimarisha uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla. Banda la wizara hiyo limepambwa na taarifa mbalimbali za kitaalamu kuhusu uongezaji thamani madini, usalama wa wachimbaji wadogo, fursa za uwekezaji, na matumizi ya teknolojia bunifu katika sekta ya madini. Akizungum...

TADB YATOA MIKOPO KWA WAZALISHAJI NA WACHAKATAJI 762,291.

Picha
  IMEELEZWA KUWAMNYORORO WA THAMANI UMEKUWA KWA WAKULIMA NA WACHAKATAJI.  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo, imefanikiwa kuwafikia zaidi ya wanufaika 762,291 nchi nzima, kwa kuwasaidia kupata mikopo kupitia taasisi za kifedha bila hitaji la dhamana kubwa. Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji Kitaifa  Rosemary  Gordon Afisa Biashara wa TADB anayesimamia mfuko huo, alieleza kuwa mfuko huo unatekelezwa kwa ushirikiano na benki 13 za biashara, benki za ushirika, na taasisi nyingine za kifedha nchini.  “Mfuko huu unahakikisha kuwa wakulima wadogo, hata wale wasio na dhamana ya kutosha, wanapata mikopo ya kuwawezesha kuendesha shughuli zao za kilimo kutoka shambani hadi sokoni,” akisema Gordon. Amesema mikopo inayodhaminiwa na mfuko huo husaidia wakulima kununua pembejeo kama mbegu, viuatilifu na mbolea, pamoja na dhana za kilim...

TAIFA STARS YAPATA MAFUNZO YA UADILIFU MICHEZONI.

Picha
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo wamepata mafunzo ya Uadilifu michezoni kuelekea mashindano ya CHAN 2024, yanayotarajiwa kuanza 02 Agosti 2025.

BEKA FRAVOUR ANOGESHA MKESHA WA MWENGE IGUNGA.

Picha
MSANII wa Mziki wa kizazi Kipya Beka Fravour ni mmoja ya Wasanii waliopanda na kutumbwiza katika jukwaa la Mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2025 katika uwanja wa mpira wa miguu wa Barafu ulio katika Kitongoji cha Kati Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.  Mwenge wa Uhuru 2025 katika uwanja wa mpira wa miguu wa Barafu ulio katika Kitongoji cha Kati Wilaya ya Igunga.