Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 17, 2026

ALIYEKUWA DED SIMANJIRO ASHINDA KESI YA PILI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Samwel Warioba Gunza ameachiwa huru na mahakama kwenye kesi ya rushwa ya shilingi milioni 5 na matumizi mabaya ya madaraka. Hata hivyo, aliyekuwa DED huyo wa Simanjiro, Gunza hakuwepo mahakamani kwani yupo magereza bado anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kesi nyingine ya rushwa alipohukumiwa mwaka 2025. Katika kesi hiyo, Gunza alifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Simanjiro, Onesmo Nicodemo na kusomewa shitaka na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU). Katika hukumu ya shauri hilo la uhujumu uchumi lililosomwa kwenye mahakama hiyo iliyopo mji mdogo wa Orkesumet, Gunza hakukutwa na hatia. Hakimu Nicodemo akisoma hukumu hiyo ameieleza  mahakama hiyo kuwa hakukuwa na ushahidi usiokuwa na mashaka wenye kumtia hatiani mshtakiwa huyo, katika makosa mawili ya rushwa  na kutumia madaraka vibaya. Amesema katika shtaka la kw...

WATU SITA WAKAMATWA KWA UTEKAJI NA MAUAJI YA BODABODA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora JESHI la Polisi Mkoani Tabora linawashikiria watu sita kwa tuhuma za kuteka na kuua mwendesha bodaboda Hamis Nchambi (27) msukuma, mkazi wa Kata ya Mbugani katika halmashauri ya manispaa ya Tabora. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, ACP Constantine Mbogambi amethibitisha kukamatwa watuhumiwa hao kutokana na msako mkali uliofanywa na Polisi katika maeneo mbalimbali baada ya kupokea taarifa za mauaji hayo. Kamanda Mbogambi ameeleza kuwa watuhumiwa hao walitumia mbinu ya mmoja wao kujifanya abiria na kukodi pikipiki hiyo siku ya tarehe 13 Januari 2026 majira ya saa 2 usiku ili impeleke nyumbani kwake. Amefafanua kuwa walipofika eneo la makaburi ya Miemba katika manispaa hiyo ghafla walimteka na kumfunga kamba shingoni, mikononi na miguuni na kisha kumnyonga ili kujipatia kipato kisicho halali. Mwili wa marehemu ulipatikana kesho yake siku ya tarehe 14 Januari 2026 majira ya saa 9.30 alasiri katika eneo la makaburi hayo, katika Kata ya Miemba, ukiwa umefungwa...