Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 25, 2025

MAANDALIZI YA KUELEKEA MIAKA 64 YA MAGEREZA YAKAMILIKA.

Picha
MAANDALIZI yamekamilika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Miaka 64 ya Jeshi la Magereza Baada ya Uhuru, ambayo yatafanyika Agosti 26, 2025 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga Dar Es Salaam, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

KEMBAKI AWATAKA WAJUMBE KUWA WATULIVU NA KUWA NA MSHIKAMANO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma  WANANCHI wa Tarime Mjini wametakiwa kuwa watulivu na kuendelea kuwa na mshikamano, kufuatia kukamilika kwa mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliolenga kumpata mgombea atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi ujao. Kauli hiyo imetolewa leo, Agousti 25 ,2025 jijini Dodoma na aliyekuwa Mbunge wa Tarime Mjini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Michael Kembaki ,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatima ya mchakato wa kura za maoni na mwelekeo wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Kembaki, ambaye amemaliza muda wake wa miaka mitano bungeni, amewashukuru wananchi wa Tarime kwa ushirikiano waliompa wakati wa uongozi wake, pamoja na wajumbe waliompa kura katika kura za maoni. Katika mchakato huo, Kembaki alipata kura ,5572,  Hata hivyo, anasema kuwa chama kilifanya maamuzi yake kupitia ngazi mbalimbali kuanzia vikao vya kata, wilaya, mkoa hadi taifa na hatimaye kumpitisha mgombea mwingine kupeperusha bendera ya ...

RAIS MWINYI ATUNUKIWA PHD YA UCHUMI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu (PhD Honoris Causa) ya Uchumi iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU), ambayo ilitangazwa rasmi Desemba 2024 katika mahafali ya Chuo hicho. Mkuu wa Chuo hicho, Mhandisi Abdulqadir Othman Hafez, alikabidhi rasmi Shahada hiyo kwa Rais Dkt. Mwinyi Ikulu Zanzibar leo tarehe 25 Agosti, 2025. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amekipongeza Chuo hicho kwa kuthamini na kutambua juhudi zake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Zanzibar, hatua ambayo ameieleza kuwa itamwongezea ari ya kuendeleza maendeleo zaidi nchini.

RAIS MWINYI AKUTANA NA WANAFUNZI WATAKAOITEMBELEA NASA, MAREKANI NA KUHUDHURIA HACKATHON, OMAN

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za kuwaandaa vijana wengi zaidi wa Zanzibar kuwa wataalamu wa elimu ya anga. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na wanafunzi watano waliochaguliwa kutembelea makao makuu ya NASA yaliyopo Washington D.C., Marekani, pamoja na kushiriki katika mashindano ya NASA International Space Apps Challenge 2025 yatakayofanyika jijini Ibra, Oman. Mkutano huo umefanyika Ikulu Zanzibar leo tarehe 25 Agosti 2025. Fursa hiyo imetokana na uwezo mkubwa waliouonesha waliposhiriki katika programu ya Kimataifa ya IASC (International Astronomical Search Collaboration) inayohusu uvumbuzi wa asteroids kwa kushirikiana na NASA (National Aeronautics and Space Administration) ya Marekani.  Jumla ya wanafunzi 22 kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait ambao ...