Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 27, 2026

VIWANDA NA BIASHARA WAPANDA MITI KUMUUNGA MKONO RAIS, DKT. SAMIA KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA.

Picha
Na Mwandishi Wetu,  Dodoma. MITI imekuwa muhimili muhimu katika ukuaji wa Sekta ya Viwanda na Biashara kwani kupitia miti, viwanda hupata malighafi, biashara hukua, na uchumi huimarika. Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb.), Januari 27, 2026, akiwa ameambatana na Naibu Waziri,Mhe. Dennis Londo pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Needpeace Wambuya kushiriki zoezi la kupanda miti katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma.  Zoezi hilo ni sehemu ya kusherehekea kumbukizi ya  siku ya kuzaliwa ya  Mwanamazingira namba moja hapa nchini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye aliazimisha siku yake 27 Januari, 1960 kwa kupanda mti wa Muembe (Mangifera indica) katika eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 27 Januari, 2026. Aidha, Waziri Kapinga wakati akiongea na Watumishi wa Wizara hiyo baada ya kupanda mti, Altria rai kwa watumishi wa wizara ...

HALMASHAURI YA IGUNGA YAUNGANA NA WATANZANIA KUPANDA MITI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Igunga. MKURUGENZI  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid ameiongoza Menejimenti ya Halmashauri hiyo kupanda miti kwa lengo la kuitekeleza 27 ya kijani iliyoasisiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Selwa ameungana na viongozi hao leo,  ikiwa ni ishara ya kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia katika kumbukizi ya kazaliwa kwake. "Kipekee ninaishukuru na kuipongeza Menejimenti kujindaa na kushiriki zoezi hili baada ya masaa ya kazi kuungana na 27 ya kijani ikiwemo kumpongeza na kumtakia kila la kheri Mheshimiwa. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan," ameshukuru.  Ameeleza kuwa wamepanda miche 70 ambapo miche 50  yakivuli huku 20 ikiwa ni ya  matunda ambayo yatawafaidisha vizazi na vizazi.

IGUWASA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS, DKT. SAMIA KWA KUPANDA MITI.

Picha
  Tabora, Januari 27, 2026. Na Lubango Mleka, Igunga. KAATIKA kuunga mkono tamko la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu upandaji wa miti kama sehemu ya utunzaji wa mazingira, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Igunga (IGUWASA) imefanya zoezi la upandaji wa miti mbalimbali katika eneo la ofisi zake. Zoezi hilo limefanyika ikiwa ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mheshimiwa Rais, ambapo taasisi hiyo imeeleza kuwa inalenga kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika kulinda na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho. Viongozi na watumishi wa IGUWASA wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Bi. Selwa  Abdallah Hamid wameshiriki katika zoezi hilo, wakisisitiza kuwa upandaji miti ni hatua muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa rasilimali za maji. IGUWASA imewahimiza wananchi kuiga mfano huo kwa kupanda ...

MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA GARI SHINYANGA 12 WAJERUHIWA

Picha
DEREVA wa Lori lenye namba za usajili RAE 848  Mali ya Kampuni ya Jaja ya nchini Rwanda amepoteza maisha baada ya kugongana uso kwa uso na basi la abiria namba T 229 EEL mali ya kampuni ya Kisire lililokuwa likitokea Kahama kwenda Mwanza na kusababisha Majeruhi 12. Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea Januari 27 katika eneo la Tinde Mnadani na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Basi la Kisire aliyetaka kupita mkokoteni uliokuwa umebeba matunda na kuhama upande mwingine na kugongana uso kwa uso na lori hilo.