MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA GARI SHINYANGA 12 WAJERUHIWA
DEREVA wa Lori lenye namba za usajili RAE 848 Mali ya Kampuni ya Jaja ya nchini Rwanda amepoteza maisha baada ya kugongana uso kwa uso na basi la abiria namba T 229 EEL mali ya kampuni ya Kisire lililokuwa likitokea Kahama kwenda Mwanza na kusababisha Majeruhi 12.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea Januari 27 katika eneo la Tinde Mnadani na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Basi la Kisire aliyetaka kupita mkokoteni uliokuwa umebeba matunda na kuhama upande mwingine na kugongana uso kwa uso na lori hilo.

Maoni