Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba 14, 2025

WAZIRI MKUU: WATANZANIA TUNZENI AKIBA YA CHAKULA

Picha
  ..Ahimiza matumizi ya mbolea na mbegu za mazao ya muda mfupi. Na Mwandishi Wetu, Dodoma. WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania watunze akiba ya chakula walichonacho na waepuke matumizi yasiyofaa kutokana na hali ya kuchelewa kwa msimu wa mvua. Waziri Mkuu ametoa wito huo leo jioni (Jumapili, Desemba 14, 2025) wakati akizungumza na baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma. Amewaeleza viongozi hao kutoka mikoa ya Dodoma na Singida kwamba Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa utabiri wa mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli na mvua za msimu kwa kipindi cha Oktoba 2025 hadi Desemba 2025 na kipindi cha mwezi Novemba, 2025 hadi Aprili 2026 mtawalia.  “Kutokana na utabiri huo, baadhi ya mikoa nchini inatarajiwa kuwa na mvua za chini ya wastani hadi wastani na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa mvua usioridhisha,” amesema.  Amesema tathmini hiyo ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaonesha hali ya...

MHE. CHANDE AWAFUNDA WAHITIMU CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI MWEKA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro. NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amewataka wahitimu wa chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, kuzingatia uadilifu, uzalendo na unyenyekevu wakati wa kuhudumia wananchi na kulinda rasilimali za wanyamapori ili kuongeza thamani katika maendeleo ya ukuaji wa sekta ya utalii kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla. Mhe. Chande ametoa wito huo mkoani Kilimanjaro wakati wa mahafali ya 61 ya chuo hicho kilichopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ambapo amewasisitiza wahitimu hao kutumia vyema maarifa na taaluma ya elimu  waliyopata kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa katika kuisaidia jamii kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kusaidia kutatua migogoro baina ya binadamu na Wanyamapori wakali na waharibifu. “Vyeti tu havitoshi, bali utekelezaji wa yale mliyojifunza na kufunzwa chuoni, hivyo  nendeni kuyaonesha kwa vitendo huko mnapokwenda, kwa sababu cheti ni karatasi lakini maarifa mliyoyapata katika...

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA LINDI MWAMBAO LTD CHAWEKA REKODI YA KUUZA TANI 41,000 ZA KOROSHO KATIKA MINADA MITANO

Picha
Na Lubango Mleka, Lindi. CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao kimeendelea kufanya vizuri katika msimu wa mauzo ya korosho baada ya kupeleka sokoni jumla ya tani 41,000 katika minada mitano iliyofanyika tangu kuanza kwa msimu huu. Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mnada wa tano uliofanyika katika Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi Mjumbe wa Bodi ya Lindi Mwambao Said Mwinyi amesema chama hicho kimeendelea kuhakikisha kuwa korosho za wanachama wake zinafika sokoni kwa wakati na kwa utaratibu unaotakiwa. Mwinyi amesema  katika minada yote mitano bei ya juu ya korosho imefikia shilingi 2,650 kwa kilo huku bei ya chini ikiwa shilingi 2,170 hatua ambayo amesema inaonesha utulivu wa soko na mwitikio mzuri kutoka kwa wanunuzi. “Hadi sasa tumeshapeleka sokoni zaidi ya tani 41,000 za korosho, jambo ambalo linaonesha uimara wa chama na maandalizi mazuri tuliyofanya. Wanachama wetu wanaendelea kunufaika na mchakato huu wa mauzo,” amesma Mwinyi.

ECOWAS YATARAJIA KUKUTANA HII LEO JIJINI ABUJA NIGERIA

Picha
JUMUIYA  ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS inatarajiwa kukutana hii leo jijini Abuja nchini Nigeria, wakati huu ikitangaza hali ya hatari ya kikanda kufuatia kuongezeka kwa uongozi wa kijeshi na majaribio ya mapinduzi katika nchi za Mali, Burkina Faso, Niger, Guinea, na njama ya hivi punde zaidi nchini Benin ikitoa tahadhari mpya.