CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA LINDI MWAMBAO LTD CHAWEKA REKODI YA KUUZA TANI 41,000 ZA KOROSHO KATIKA MINADA MITANO
CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao kimeendelea kufanya vizuri katika msimu wa mauzo ya korosho baada ya kupeleka sokoni jumla ya tani 41,000 katika minada mitano iliyofanyika tangu kuanza kwa msimu huu.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mnada wa tano uliofanyika katika Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi Mjumbe wa Bodi ya Lindi Mwambao Said Mwinyi amesema chama hicho kimeendelea kuhakikisha kuwa korosho za wanachama wake zinafika sokoni kwa wakati na kwa utaratibu unaotakiwa.
Mwinyi amesema katika minada yote mitano bei ya juu ya korosho imefikia shilingi 2,650 kwa kilo huku bei ya chini ikiwa shilingi 2,170 hatua ambayo amesema inaonesha utulivu wa soko na mwitikio mzuri kutoka kwa wanunuzi.
“Hadi sasa tumeshapeleka sokoni zaidi ya tani 41,000 za korosho, jambo ambalo linaonesha uimara wa chama na maandalizi mazuri tuliyofanya. Wanachama wetu wanaendelea kunufaika na mchakato huu wa mauzo,” amesma Mwinyi.



Maoni