Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 4, 2026

MAKAMU WA RAIS BALOZI DKT. NCHIMBI AMWAKILISHA RAIS. DKT. SAMIA KWENYE MAZISHI YA MBUNGE WA VITI MAALUMU TABORA MUNDE TAMBWE.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Tabora. MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mbunge wa Viti Maalum Mstaafu, Marehemu Munde Tambwe, yaliyofanyika Mkoani Tabora, leo tarehe 04 Februari 2026. Akitoa salamu za rambirambi katika msiba huo, Makamu wa Rais amesema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufuatia msiba huo mkubwa. Amesema mchango wa Marehemu Munde Tambwe ni wa kipekee sana ndani ya Taifa pamoja na Chama Cha Mapinduzi. Makamu wa Rais amesema marehemu Munde aliweka mbele maendeleo ya nchi na Chama Cha Mapinduzi na wakati wote alikuwa rafiki wa kila mtu alijali sana uhusiano mzuri. Ameongeza kwamba kufuatia marehemu Munde kuanzisha ujenzi wa msikiti ambao utahitaji ukamilishaji, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha shilingi milioni 30 zitakaz...

POLISI MWANZA YAKANUSHA TAARIFA ZA UWEPO WA VIKUNDI VYA KIHALIFU NA UASI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza. JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza limetoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zenye kichwa cha habari kinachoeleza kuwa “kundi la uasi laibuka Mwanza, Polisi waonekana mitaani.” Kulingana na Taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Wilbrod Mutafungwa amesema taarifa hizo ni za upotoshaji zikiwa na lengo la kuleta taharuki kwa jamii, kwani wahalifu wa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wamekuwa wakichukua picha za askari na vitendea kazi vyao kisha kutengeneza maudhui yenye lengo la kuzua taharuki, kuchonganisha na kupandikiza chuki.  "Jeshi la Polisi linawasisitiza wananchi kuendelea kuwapuuza watu kama hao wanaosambaza taarifa zenye nia ovu na badala yake wafuatilie na kupata taarifa zenye ukweli na usahihi kutoka kwenye mamlaka zenye jukumu la kufanya hivyo." Amesema Kamanda Mutafungwa. Aidha, Jeshi la Polisi limesema linaendelea kuwafuatilia kwa karibu watu wo...

NUKUU ZA LEO KUTOKA WIZARA YA AFYA

Picha

WANANCHI WATAKIWA KUZINGATIA MIPANGO YA MATUMIZI BORA YA ARDHI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma WANANCHI wametakiwa kuzingatia mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kukidhi mahitaji ya sasa na baadaye katika shughuli za kilimo, ufugaji na makazi ili kuendelea kulinda na kuhifadhi maeneo yakiyohifadhiwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.  Hayo yamesemwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), katika kikao cha 7 cha Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu swali la Mhe. Onesmo Merdson Mnkondya (Mb), aliyehoji kuhusu mpango wa Serikali kuwapa kipande cha ardhi Wananchi wanaozunguka Hifadhi ndogo ya Isalalo iliyo chini ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS). Mhe. Chande amefafanua kuwa hifadhi ya msitu Isalalo ilianzishwa kwa ajili ya kuhifadhi vyanzo vya maji, mimea na wanyama, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuhifadhi udongo kwa kuwa msitu huo unazungukwa na jamii ya vijiji vitano ikiwemo Itentula na Hamwelo, Nambizo, Ipapa, na Utambalila am...

SERIKALI YATOA FEDHA BILIONI 19. 513 KUPELEKA UMEME KWENYE VITONGOJI 127 ARUSHA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Arusha. MKUU wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amesema Shilingi 19,513,813,347 zimetolewa ili kusambaza umeme kwenye Vitongoji 127 vya Majimbo sita ya Mkoa wa Arusha ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan ya kufikisha umeme kwenye Vitongoji vyote Mkoani Arusha mara baada ya kuwa Serikali imefikisha umeme kwenye Vijiji vyote 368. Mhe. Makalla amebainisha hayo leo Jumanne Februari 04, 2026 Ofisini kwake Jijini Arusha alipotambulishwa Mkandarasi Nakuroi Investment Company Ltd, atakayetekeza mradi wa usambazaji umeme katika Vitongoji hivyo 127 kutoka katika Wilaya zote za Arusha. “Kikubwa kwaniaba ya Wakuu wa Wilaya niwahakikishie ushirikiano Tanesco pamoja na Mkandarasi anayetekeleza mradi huu na niagize Mradi mmoja unapokamilika, uzinduliwe wananchi waanze kufaidika. Niagize pia kutumika kwa Vijana wa maeneo husika ili wapate ajira wakati wa utekelezaji wa mradi huu wa Umeme.” Amesisitiza Mhe. Makalla. Kwa upande wake Mhandisi Er...

NAIBU KATIBU MKUU CCM AONGOZA MAZISHI YA MNEC TABORA

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora. NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Mongella ameongoza umati wa wanaCCM na wakazi wa Tabora kumzika  aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mzee Nassoro Hamdan Seif. Akitoa salamu za chama kwenye ibada ya mazishi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Mongella amemwelezea Mzee Hamdan kuwa ni Kiongozi aliyekitumikia chama kwa moyo wake wote hali iliyopelekea kuaminiwa na wanaCCM wote. ‘Ndugu zangu wana Tabora nachukua nafasi hii kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt Asha-Rose Migiro kuwapa pole nyingi kwa kuondokewa na Mzee wetu, aliyekuwa Kada mwaminifu na nguzo muhimu ya Chama chetu’, ameeleza. Mongella amebainisha kuwa enzi za uhai wake marehemu amefanya kazi kubwa ya kukiimarisha Chama na kukiwezesha kuibuka kidedea katika chaguzi za Urais, Ubunge na Udiwani na Serikali za Mitaa. Ametoa wito kwa wanaCCM kuyaenzi mazuri yote aliyoyafanya alipokuwa Kiongozi katika nafasi mbalimbali na kuongeza kuwa umati mkubwa uliojitokeza kumsin...

UWT TABORA WAMLILIA MUNDE TAMBWE

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora. UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoani Tabora wamepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa huo kupitia Jumuiya hiyo Bi.Munde Tambwe aliyefariki dunia juzi jijini DSM. Akizungumza na gazeti hili jana Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Tabora Rhoda Madaha ameeleza kuwa marehemu alikuwa nguzo muhimu sana kwa maendeleo ya wanawake wote wa Mkoa huo. ‘Marehemu alikuwa mstari wa mbele kuhamasisha wanawake na Vijana wa Wilaya zote za Mkoa wetu kuanzisha miradi ya kiuchumi ili kujikwamua kimaisha na alikuwa anatenga bajeti yake kuwawezesha’, ameeleza. Madaha amebainisha kuwa enzi za uhai wake, marehemu alikuwa karibu zaidi na wanawake na kila akirudi kutoka bungeni alikuwa na agenda moja tu ya kukutana na makundi mbalimbali ya akinamama na kusikiliza kero zao. Ameongeza kuwa ukarimu na ukaribu wake kwa wanawake ulimpa kibali sana ndio maana amekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa awamu nne za miaka mitano mitano na katika uchaguzi mkuu...

MADIWANI SIMANJIRO WAMPONGEZA OLE MILLYA

Picha
   Na Mwandishi Wetu, Simanjiro. MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Simanjiro James Ole Millya kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Kaleiya Mollel akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani kilichofanyika mji mdogo wa Orkesumet amesema wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Ole Millya kushika nafasi hiyo. "Tangu dunia iumbwe ni mara ya kwanza Simanjiro kutoa Naibu Waziri hivyo tumpe ushirikiano wa kutosha ili aweze kuitumikia vyema nafasi hiyo ambayo Rais Samia ameona inamfaa katika kuitumikia," amesema Kaleiya.  Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mwanjaa Jacob amesema Ole Millya amewapa heshima kubwa watu wa Simanjiro hivyo watamuunga mkono ili aitumikie nafasi hiyo ipasavyo.  "Mbunge wetu ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, hii ni heshima...