WAKAZI USUNGA WAFURAHIA MRADI WA MAJI
Na Allan Kitwe, Sikonge. WAKAZI wa Kijiji Cha Usunga, Kata ya Usunga Wilayani Sikonge Mkoani Tabora wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea mradi wa maji safi na salama ya kunywa. Wametoa shukrani hizo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 58 tangu kuanzishwa kwa Kijiji hicho zilizofanyika jana kwenye uwanja wa CCM (Centre) na kueleza bayana kuwa serikali imemaliza kilio chao cha muda mrefu. Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho James Mgulu ameeleza kuwa mradi wa maji katika Kijiji hicho umeleta neema, furaha na shangwe kwa wananchi kwa sababu familia zao zilikuwa zinapata shida sana kwa kukosa maji safi na salama. ‘Tuna kila sababu ya kuishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea mradi huu wa maji na miradi mingine ya maendeleo, wananchi sasa wana amani tele, na maisha yao yamekuwa bora zaidi’, ameeleza. Ameongeza kuwa wanapoadhimisha sherehe hiyo kila mwaka wanalenga kudumisha mila, utamad...