Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 23, 2026

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA ALAT TAIFA

Picha
  Na Mwandishi Wetu.  MSTAHIKI Meya wa Jiji la Mwanza amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Association of Local Authorities of Tanzania (ALAT) Taifa, baada ya kujizolea jumla ya kura 273 kati ya kura 339 zilizopigwa. Katika uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali, jumla ya wagombea wanne walijitokeza kuwania nafasi hiyo muhimu ya uongozi wa mamlaka za serikali za mitaa nchini.  Hata hivyo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza aliibuka mshindi kwa kupata kura nyingi zaidi, akionesha imani kubwa waliyonayo wajumbe wa ALAT Taifa kwake. Ushindi huo unaashiria heshima na imani kwa uongozi wa Jiji la Mwanza katika kusimamia na kuendeleza masuala ya maendeleo ya serikali za mitaa nchini.  Aidha, ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya halmashauri mbalimbali na kuendeleza ajenda za maendeleo kwa wananchi. Kupitia nafasi hiyo mpya, Mstahiki Meya anatarajiwa kusimamia na kuratibu shughuli za ALAT Taifa, ikiwa ni pamoja na kutetea maslahi ya mamlaka...

HAWA MWAIFUNGA AAHIDI TABASAMU KWA WAKAZI MANISPAA TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  MBUNGE wa Jimbo la Tabora Mjini Hawa Subira Mwaifunga amefanya mkutano mkubwa wa hadhara Jimboni humo na kupokea kero za wananchi huku akiahidi kuwapa tabasamu kwa mazuri yatakayofanyika. Ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika uwanja wa TBC ulio karibu na Ofisi za CCM Tabora Mjini ambapo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi na wana CCM wote kwa kumchagua kuwa mbunge wao. Mwaifunga amesema kuwa kuanzia sasa ataanza utaratibu wa kupita mtaa kwa mtaa, kata kwa kata ili kupokea mawazo ya nini wananchi wanataka, kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka na wa kudumu. Amefafanua kuwa mbunge ni mtumishi wa wananchi, hivyo ana wajibu wa kutembelea, kusikiliza na kutatua kero na shida za wananchi wake kwa kuwa ndio waliompeleka bungeni. ‘Mbunge na diwani wanawajibika moja kwa moja kwa waliowachagua, kwa kuhakikisha wanajua kero zao na kuzitafutia ufumbuzi, kazi yetu ni kuwapa tabasamu wananchi na si vinginevyo,’ a...

MALIASILI NA UTALII WATATHMINI UTENDAJI WA ROBO TATU MWAKA DODOMA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WATAALAMU wa Ufuatiliaji na Tathimini wa Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake wamekutana katika Kikao kazi cha Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kwa ajili ya Maandalizi ya Taarifa ya Ufuatiliaji na Utendaji Kazi wa Wizara kwa Kipindi cha Robo Tatu Mwaka (Julai, 2025 hadi Machi, 2026) katika Ukumbi wa TANAPA jijini Dodoma. Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Bure Nassibu amesema kuwa lengo la kikao hicho ni Kujadili na Kuandaa Taarifa ya Ufuatiliaji wa Utendaji Kazi wa Wizara kwa kipindi cha Robo Tatu (Julai, 2025 – Machi, 2026) kwa kuzingatia viwango vya ubora na ushahidi wa utekelezaji. Bi Bure aliongeza kuwa kikao hicho kinaongozwa na Kaulimbiu ya Kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini kwa Matokeo Endelevu ya Utekelezaji wa Sera, Mipango na Miradi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026. Aidha, Wataalamu hao watafanya mapitio ya utekelezaji wa shughuli za Wizara ikiwemo kupima hatua iliyofik...