Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 6, 2026

KAPINGA: DHANA YA TAKA SIFURI INAFUNGUA FURSA ZA BIASHARA NA VIWANDA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Istanbul-Ururuki.  WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amesema dhana ya taka sifuri na urejeshaji bidhaa ni fursa muhimu ya kukuza sekta ya viwanda, kuongeza thamani ya malighafi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza katika kikao cha mawaziri kilichofanyika jijini Istanbul nchini Uturuki, Juni 5, 2026, kilichobeba mada ya Mageuzi ya Kijani ya Viwanda, Mtazamo wa taka sifuri na urejeshaji bidhaa, Kapinga amesema Tanzania inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta ya viwanda huku ikisisitiza matumizi bora ya rasilimali na uhifadhi wa mazingira. Ameeleza kuwa dhana ya taka sifuri na urejeshaji bidhaa inatoa fursa kwa nchi zinazoendelea kupitia matumizi endelevu ya malighafi, kupunguza upotevu baada ya mavuno, kupunguza uzalishaji wa taka na kuongeza thamani ya bidhaa zinazotengenezwa viwandani. Kapinga amesema Serikali ya Tanzania imeendelea kuunganisha masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika s...

OLE MILLYA AKEMEA UUZWAJI ARDHI SIMANJIRO

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani.  NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki James Ole Millya ambaye pia ni Mbunge wa Simanjiro Mkoani Manyara, amekemea vikali uuzwaji holela wa ardhi unafanywa baadhi ya viongozi wa vijiji. Ole Millya ameyasema hayo katika Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro, kwenye ziara ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Laban Kihongosi alipohitimisha ziara yake ya siku tatu Mkoani Manyara. Amesema tatizo la uuzwaji holela wa ardhi katika wilaya ya Simanjiro, limekuwa kero kwani baadhi ya viongozi wa vijiji wenye tamaa wanagawa ardhi kwa maslahi yao  "Baadhi ya wenyeviti wanauza ardhi bila kushirikisha mkutano mkuu wa kijiji na baadhi ya wenyeviti wastaafu wanatembea na mihuri na mihutasari iliyopita katika uuzaji wa ardhi," amesema Ole Millya. Ameeleza kwamba wakati mwingine anaona ni vyema hata miradi ya maendeleo isifanyike kwa muda wa mwaka mmoja ili viongozi na jamii kwa ujumla ishuhulikie migogoro ya ar...

MATHIAS CANAL ATWAA TUZO YA USHIRIKI BORA WA KAZI ZA JAMII 2026

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  MWANZILISHI na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za WAZOHURU MEDIA na WAZOHURU APPARTMENTS, Mathias Canal, ametunukiwa Tuzo ya Ushiriki Bora wa Kazi za Jamii 2026, ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika kuhamasisha maendeleo ya jamii kupitia shughuli mbalimbali za kijamii na misaada ya kijamii. Tuzo hiyo iliyotolewa usiku wa Juni 5, 2026 jijini Dodoma katika hafla ya utoaji wa tuzo iliyoandaliwa na Central Zone Awards, tukio lililowakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta tofauti waliotoa mchango wa kipekee katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Waandaaji wa tuzo hizo wamesema Mathias Canal amestahili kutunukiwa tuzo hiyo kutokana na kujitolea kwake, ushiriki wake wa karibu na jamii pamoja na mchango wake endelevu katika kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji.  Tuzo hiyo pia imetambua moyo wake wa huruma, uwajibikaji na dhamira ya kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wananchi. Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mathia...