MELI KUBWA MPYA YA KISASA YAWASILI BANDARI YA DAR ES SALAAM
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. MELI ya Grande Shanghai kutoka nchini China imetia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam usiku wa tarehe 20 Septemba, 2025. Meli hiyo maalum kwa ajili ya kubeba magari, ni mpya kabisa ambayo imetengenezwa mwaka 2025 inatumia nguvu ya umeme jua (solar power) ambayo ni teknolojia rafiki kwa mazingira badala ya kutumia mafuta katika uendeshaji wake. Meli hiyo ya ghorofa 14 na urefu wa mita 220 ina uwezo wa kubeba magari 9,000 kwa wakati mmoja. Kwa sasa meli hiyo inaendelea na ushushaji wa magari 1624 katika Bandari ya Dar es Salaam. Wakizungumza wakati wa hafla fupi ya upokeaji wa meli hiyo, kwa niaba ya menejimenti ya meli hiyo, Bw. Girolamo Carignani amesema: “huu ni mwanzo kwa meli zetu kufika katika Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania." Amesema kuwa wataendelea kufanya safari za kuja nchini Tanzania ili kuboresha biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine, na kuongeza kuwa hivi karibuni itaanza safari za kwenda Japan kutokea Ch...