Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 24, 2026

SERIKALI YAIMARISHA UPATIKANAJI WA MAFUTA YA PETROLI NCHINI MALAWI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SERIKALI kupitia Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuwa nguzo muhimu ya upatikanaji wa mafuta kwa nchi jirani ya Malawi, hatua inayochochea shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi wa nchi hizo mbili. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miundombinu ya mafuta katika Kituo cha Kurasini Oil Jet (KOJ-1), kilichopo katika Bandari ya Dar es Salaam leo Machi 24, 2026, Waziri wa Nishati na Madini wa Malawi, Mhe. Dkt. Jean Mathanga, aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika kuwezesha mtiririko wa mafuta kwenda nchini Malawi. Alisema kuwa kutokana na Malawi kutokuwa na bandari, nchi hiyo inategemea kwa kiasi kikubwa miundombinu ya nchi jirani, hususan Tanzania, katika kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unaendelea kuwa wa uhakika. Alibainisha kuwa ziara hiyo imelenga kujionea kwa vitendo namna mafuta yanavyopokelewa na kusimamiwa bandarini ili kuboresha mipango ya ununuzi na usambazaji wa mafuta nchini Malawi.  Kwa ...

TAFITI ZAENDELEA KUTUMIKA KATIKA MAAMUZI YA SERA KUPITIA PORTAL MPYA YA SERIKALI

Picha
  Na Jasmine Shamwepu,Dodoma HATUA ya Serikali kuanzisha mfumo wa kidijitali wa kukusanya na kusambaza tafiti mbalimbali nchini, inatarajiwa kuleta mapinduzi katika matumizi ya ushahidi wa kisayansi kwenye maamuzi ya sera na mipango ya maendeleo. Kupitia portal hiyo mpya, matokeo ya tafiti yaliyokuwa yakibaki kwenye makabrasha au kuhifadhiwa ndani ya taasisi, sasa yatapatikana kwa urahisi na kutumiwa moja kwa moja na watunga sera, wataalamu pamoja na wadau wa maendeleo. Akizungumza Machi 23, 2026 jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kitaifa wa taasisi za utafiti, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, amesema mfumo huo ni sehemu ya mageuzi ya kimkakati ya kuifanya Tanzania kuwa taifa linaloongozwa na ushahidi katika kufanya maamuzi. Ameeleza kuwa portal hiyo itaongeza uwazi, kuimarisha ushirikishwaji wa wadau na kuhakikisha tafiti zinatumika kutatua changamoto halisi za wananchi. “Mfumo huu utasaidia kuungan...