Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 30, 2026

RUJAT YATAKA MABADILIKO YA UANDISHI, YAANGAZA ZAIDI VIJIJINI

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Arusha MWENYEKITI  wa Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini Tanzania (RUJAT), Neville Meena, amesema kuwa ni muhimu kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari huku ikiwekewa mkazo sauti ya wananchi wa vijijini ili kuhakikisha hakuna kundi linaloachwa nyuma katika upatikanaji wa taarifa. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika jijini Arusha, Meena amesema uhuru wa vyombo vya habari unapaswa kuambatana na uwajibikaji wa kitaaluma kwa wanahabari kuzingatia misingi ya ukweli, usahihi, uwiano na maslahi ya umma. Maadhimisho hayo yaliyowakutanisha wadau wa sekta ya habari kwa siku mbili katika Hoteli ya Mount Meru, yalijadili mustakabali wa tasnia ya habari katika muktadha wa mabadiliko ya kidijitali, yakilenga pia kukuza ubunifu na kuhakikisha uendelevu wa taaluma ya uandishi wa habari. Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa RUJAT, Prosper Kwigize, amesema chama hicho kimejipanga kushirikiana na taasisi mbalimb...

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUJITEGEMEA KIUCHUMI KUEPUKA USHAWISHI

Picha
  Na Hamida Ramadhan,Arusha.  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amewataka waandishi wa habari nchini kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi ili kuepuka kushawishiwa na wanasiasa wasio waadilifu pamoja na wala rushwa. Akizungumza jijini Arusha wakati wa kufunga maadhimisho kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Makonda alisema uhuru wa habari hauwezi kuwa kamili bila uhuru wa kiuchumi kwa wanahabari. Alisema baadhi ya waandishi wamekuwa wakiandika habari kwa maslahi ya wanasiasa, hali ambayo ni hatari kwa mustakabali wa taaluma ya habari na inaweza kupotosha jamii. “Ni muhimu kwa mwandishi wa habari kuwa na uhuru wa kiuchumi ili aweze kufanya kazi yake bila hofu, upendeleo au shinikizo kutoka kwa watu wenye maslahi binafsi,” amesema Makonda. Ameongeza kuwa kuna watu wasiokuwa waaminifu wanaowashawishi waandishi kwa maslahi yao, na kusisitiza umuhimu wa wanahabari kuzingatia maadili ya taaluma yao pamoja na kuandika habari zinazojenga taif...