Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 18, 2025

ADAKWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJITEKA

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora JESHI la Polisi Mkoani Tabora linamshikilia Hadija Jimmy Mrijo (39) mpare, kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kuwa ametekwa na watu wasiojulikana ili ajipatie fedha isivyo halali kutoka kwa mume wake. Kamanda wa Polisi Mkoani hapa SACP Richard Abwao amethibitisha kushikiliwa mwanamke huyo ambaye ni mke wa Emanuel Peter Charles mkazi wa Tabora Mjini. Amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa mumewe kuwa alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akidai kuwa wamemteka hivyo awatumie fedha kiasi cha sh mil 2 ili wamwachie. Amedokeza kuwa mume wa mtuhumiwa baada ya kupokea taarifa hiyo na kusikia mlio wa kuteswa aliingiwa na hofu na kuanza kutafuta kiasi hicho cha fedha ambapo alifanikiwa kutuma kiasi cha sh 1,385,800/-. Kamanda Abwao amefafanua kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kina tumebaini kuwa mtuhumiwa hakuwa ametekwa ila alijiteka mwenyewe ili apate fedha hizo, akishirikiana na wenzake na wote wamekamatwa.  Ametaja watuhumiwa wengine ...

MATUKIO KATIKA PICHA

Picha
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji leo Novemba 18,2025 Ikulu jijini Dodoma.

WADAU WA UTALII NA UHIFADHI NYANDA ZA JUU KUSINI WAHAMASISHWA KUWANIA TUZO ZA SERENGETI

Picha
  Na Mwandishi Wetu - Iringa  WADAU wa uhifadhi na utalii  katika mikoa ya nyanda za juu kusini wamehamasishwa kushiriki katika tuzo za uhifadhi na utalii za Serengeti (Serengeti Awards 2025) zinazotarajiwa kufanyika mwezi Desemba 2025. Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utalii, Bi. Dainess Kunzugala amesema hayo leo katika kikao na wadau hao wakiwemo makampuni na waendeshaji wa shughuli za utalii , waongoza watalii , watoa huduma za malazi , wahifadhi na mashirika au taasisi zenye mchango katika uhifadhi  kilichofanyika Novemba 17, 2025 Mkoani Iringa. "Natoa hamasa kwa wadau wetu wa utalii kutumia fursa hii muhimu kutuma maombi yao kuwania tuzo hizi muhimu ambapo kuna kategoria zipatazo saba ambazo zimeainisha makundi mbalimbali" amesema Bi. Kunzugala. Amesema lengo ni kutambua mchango wa wadau hao pamoja na kuifanya sekta ya utalii iwe na mwamko katika kuleta maendeleo nchini. Naye, Mwongoza Watalii kutoka kampuni ya Mukuta Travel and Tours, Bw.Fadhili Laizer ameishukur...