Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 30, 2026

WAGONJWA 2000 KUFANYIWA UPASUAJI WA MABUSHA, MILIONI 992 KUTUMIKA. ‎

Picha
  ‎Na Hamida Ramadhan, Dodoma. ‎SERIKALI imepanga kufanya upasuaji wa mabusha kwa wagonjwa 2,000 katika mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo hadi sasa wagonjwa 1,700 wamepangiwa kufanyiwa upasuaji kwa gharama ya shilingi Milioni 992, fedha zinazotolewa na Serikali. ‎Hayo yameelezwa leo Ijumaa, Januari 30, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Duniani. ‎Waziri Mchengerwa amesema walengwa wa huduma hiyo watatoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Pwani, Morogoro na Mbeya. ‎Amesema Serikali, kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, itaendelea kutoa huduma kwa wananchi wanaoathirika na magonjwa hayo, ikiwemo huduma za upasuaji. ‎“Katika mwaka wa fedha 2024/2025, jumla ya wananchi 1,084 wamepatiwa huduma ya upasuaji wa mabusha nchini,” amesema Mchengerwa.

RIDHIWANI:HAKUTAKUWA NA MABADILIKO YA VITUO VYA KAZI KWA WAAJIRIWA WAPYA

Picha
  Na Hamida Ramadhan,  Dodoma. SERIKALI imetangaza kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa waajiriwa wapya waliopata ajira katika zoezi la ajira 12,000, ikieleza kuwa nafasi hizo zilitolewa kulingana na mahitaji halisi ya kila Halmashauri na mwajiri husika. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma,kuhusu ahadi za Siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amesema kuruhusu mabadiliko ya vituo vya kazi kutasababisha upungufu wa watumishi katika maeneo yaliyopangiwa na kuathiri utoaji wa huduma kwa wananchi. Ridhiwani amesema Serikali imefanya upangaji wa ajira hizo kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kila Halmashauri inanufaika kulingana na uhitaji wake, hivyo waajiriwa wapya wanapaswa kwenda kufanya kazi katika vituo walivyopangiwa bila masharti. Amesisitiza kuwa waajiriwa wote wapya wanapaswa kuripoti katika vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 tangu kupokea barua za...

PBPA YAFUNGUA MILANGO KWA VIJANA WA UHANDISI WA MAFUTA KUTOKA UDSM NA DMI

Picha
Na Mwandishi Wetu- Dar es Salaam. WAKALA wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) leo tarehe 30 Januari, 2026 umepokea ugeni wa wanafunzi 30 wa Kitengo cha Petroleum Engineering kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), chini ya Chama cha wahandisi wa mafuta (Society of Petroleum Engineers -SPE),waliotembelea Wakala huo kwa lengo la kujifunza kwa vitendo kuhusu utendaji kazi wa PBPA na namna Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (BPS) unavyotekelezwa nchini. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Lojistiki za Mafuta PBPA, Mhandisi Sophia Kidimwa, alisema kuwa wanafunzi hao wamepata fursa ya kuelewa mchakato mzima wa upatikanaji wa mafuta nchini kuanzia hatua za uagizaji hadi usimamizi wa lojistiki za kupokea mafuta. “Tumepokea ugeni wa wanafunzi wa mwaka wa nne kutoka UDSM na DMI waliokuja kujifunza kuhusu taratibu zote za upatikanaji wa mafuta hapa Tanzania, jinsi mafuta yanavyoingia nchini, mchakato mzima wa uletaji wake pamoj...

MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUONGEZEKA MARA.

Picha
  Majiko banifu 8,486 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Mara, Wilaya Sita kunufaika na mradi. Na Mwandishi Wetu, Mara. SERIKALI ya Mkoa wa Mara kupitia Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mara   ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji, Mhandisi Mwita Chacha Okayo leo Januari 30, 2026 imepokea mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku. Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa ya mradi, Mhandisi Mwandamizi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Deusdedith Malulu amesema, Kupitia tafiti iliyofanyika mwaka 2016 inakadiria  kuwa takribani watu 33,024 hufariki kabla ya wakati kila mwaka kutokana na magonjwa ambayo yanachangiwa na uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba wakati wa upikaji kwa kutumia nishati isiyo  safi na salama ya kupikia na hii ni sawa na asilimia 8.49 ya vifo vyote nchini. Hivyo, kwa kutambua hilo Serikali kupitia REA imekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku ili kupunguza a...

MSTAHIKI MEYA AWANYOSHEA KIDOLE WASIOENDELEZA VIWANJA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora. MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Manispaa Tabora Ghullam Hussein Dewj amewataka wananchi wote wenye viwanja katika maeneo mbalimbali ndani ya manispaa hiyo kuviendeleza ili Mji huo uonekane vizuri zaidi. Ametoa rai hiyo alipokuwa akiongea na Wataalamu, Watendaji na Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kwenye kikao cha madiwani ambako alielekeza wahusika wote kuandikiwa barua ya kukumbushwa kuendeleza maeneo yao. Amedokeza kuwa manispaa hiyo inakua kwa kasi kubwa sana kutokana na kazi nzuri ya utekelezaji miradi ya maendeleo inayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. ‘Mji wetu umeendelea kuboreshwa zaidi, lakini baadhi ya maeneo kuna viwanja havijaendelezwa, hali inayosababisha maji kutuama na kusababisha mafuriko, tunataka viwanja vyote viendelezwe, wahusika wakumbushwe’, ameagiza. Aidha Mstahiki Meya amewataka kufuatilia maeneo yote ambayo hayajapangwa vizuri ili utaratibu wa kuyafany...

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HOSPITALI YA RUFAA YA NKINGA

Picha
  HOSPITALI ya Rufaa ya Nkinga, iliyopo wilaya ya Igunga mkoani Tabora, pembezoni mwa barabara kuu ya Mwanza - Dodoma - Dar es Salaam (km 21 kutoka barabarani),  Inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa, Uadilifu na Moyo wa kuhudumia jamii, kujaza nafasi za kazi zifuataazo. (1) Daktari Daraja II - Nafasi 5 (2) Afisa Muuguzi II (Nursing Officer II) - Nafasi 3 (3) Afisa Muuguzi Msaidizi II (Assistant Nursing Officer II) - Nafasi 10 (4) Muuguzi wa Usingizi II (Nurse Anaesthesia II) - Nafasi 2 (5) Mteknolojia Mionzi Daraja II (Radiographer II) - Nafasi 2 JINSI YA KUTUMA MAOMBI Waombaji wote watume barua ya maombi iliyoambatanishwa na: • Wasifu binafsi (CV) • Nakala za vyeti vya kitaaluma na Sekondari • Cheti Cha kuzaliwa • Cheti cha usajili na leseni ya kazi • Nakala ya Kitambulisho Cha NIDA Nyaraka zote ziwe katika mfumo wa PDF MAOMBI YATUMWE KWA👇 Mkurugenzi Mtendaji  Hospitali ya Rufaa ya Nkinga  S.L.P 1, Nkinga, Igunga - Tabora  Simu: 0784800...

TEKNOLOJIA MPYA YA KUVUNA SENENE YA KISASA YABUNIWA NA SERIKALI

Picha
Na Hamida Ramadhan,  Dodoma. SERIKALI kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO), kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na VETA, imeendelea kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kuendeleza na kuboresha biashara ya senene katika mkoa wa Kagera.  Hayo yamebainishwa leo Januari 30,2026 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo wakati akijibu swali la Mbunge wa Bukoba Mjini Mha. Johnston Mutasigwa aliyehoji, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia wauza senene masoko na vifaa bora vya kutegea senene. "Mpaka sasa, teknolojia rahisi ya mfano (prototype) itakayosaidia katika uvunaji wa senene imebuniwa na kutengenezwa,"amesema. Aidha, ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutafuta na kufungua masoko ya uhakika kwa bidhaa za senene.  "Hii inajumuisha kuwaunganisha wafanyabiashara wa senene na masoko ya miji mikubwa nchini, kuwashirikisha katika maonesho ya biashara ya kitaifa na kikanda, na kutangaza senene...

FURSA MPYA KWA VIJANA: BILIONI 2 KWA WATENGENEZAJI WA MAUDHUI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma. WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda, amesema Wizara imepatiwa kiasi cha TZS bilioni 2 itakayowawezesha watengenezaji wa maudhui mbalimbali mitandaoni kuimarisha kazi zao na kuwaongezea kipato kupitia majukwaa ya kidijitali. Amesema hayo Januari 29, 2026 jijini Dodoma na kubainisha kuwa, fedha hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuyawezesha makundi yote ya watengeneza maudhui ikiwemo katika Sekta ya Utalii, Michezo, Habari, Jamii, Muziki, Filamu na sanaa nyinginezo.  Amebainisha kuwa, zoezi la uandikishaji wa walengwa linaanza rasmi Januari 30 hadi Februari 15, 2026, ambapo watengenezaji wa maudhui wanatakiwa kufika katika ofisi za Halmashauri za Wilaya, Manispaa za Miji na Majiji kupitia vitengo vya habari, ili kuchukua na kujaza fomu za maombi, zikiainisha taarifa binafsi pamoja na shughuli wanazozifanya.

"MILANGO IPO WAZI KWA UMIKIDO ", WAZIRI MAKONDA

Picha
Na Hamida Ramadhan,  Dodoma. KATIKA  kuendelea kuimarisha umoja na kujitambulisha kwa Mamlaka mbalimbali, Mwenyekiti wa Umoja wa Vyombo vya Habari Mitandaoni Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO), Benny Majata, amefanya mazungumzo mafupi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo Januari 29, 2026 Katika mazungumzo hayo, sambamba na kujitambulisha kwa Waziri Makonda, Majata amemweleza kuhusu malengo ya kuanzishwa kwa UMIKIDO, ikiwemo kusimamia maudhui yenye weledi, kuhamasisha maadili ya habari mtandaoni, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na Serikali. Kwa upande wake, Waziri Makonda amesema milango ya Wizara ipo wazi kwa UMIKIDO kufika ofisini kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kina juu ya namna Wizara itakavyoweza kusaidia umoja huo kutimiza malengo yake.

MAJIKO BANIFU MKOMBOZI WA AFYA NA MAZINGIRA SIMIYU.

Picha
  Majiko banifu 6,236 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku, Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku TZS 6,195. Na Mwandishi Wetu, Simiyu. WAKAZI wa mkoa wa Simiyu waaswa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi na salama ya kupikia. Rai hiyo imetolewa  tarehe 29 Januari , 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha wakati wa upokeaji wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku mkoani hapo. "Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za upatikanaji na uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia katika kutunza na kuhifadhi mazingira" alisema Mhe. Macha. Mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni muendelezo wa  juhudi za serikali  katika kutunza mazingira na kuboresha afya za  wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia Aliendelea kwa kuse...