Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 6, 2026

WAFANYABIASHARA KARIAKOO WAPO TAYARI KWA MFUMO WA IDRAS

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. WAFANYABIASHARA wameukubali mfumo wa Usimamizi wa Kodi za ndani (IDRAS) ,huku wakijiandaa kuupokea Jumatatu ya tarehe 9 Februari mwaka huu. Akizungumza leo 6.2.2026 jijini Dar es salaam katika mafunzo ya mfumo mpya kwa wafanyabiashara wa Kariakoo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK) Bw. Severin Mushi amesema wapo tayari kuanza kuutumia mfumo huo kwa ushirikiano wa karibu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Mwenyekiti huyo amesema kupitia mafunzo ambayo wamepatiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanaamini mfumo utakuwa msaada kwao na kuondoa changamoto mbalimbali ambazo zilikuwepo. Amesema mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara kwa kuwa yameondoa hofu iliyokuwepo awali na kuwapa uelewa wa pamoja kuhusu matumizi ya mfumo huo. Bw. Mushi amesema wamejiandaa kuupokea mfumo wa IDRAS, akieleza kuwa jambo lolote jipya huwa linaogopesha kwa wanaolipokea. Amebainisha kuwa mabadiliko ya kiteknolojia hayaepukiki ka...

TANZANIA, UNITAID KUIMARISHA UZALISHAJI WA BIDHAA ZA AFYA NCHINI

Picha
Na WAF, Geneva. MGANGA Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe,  ametumia fursa ya mkutano wa 158 wa Bodi Tendaji ya Shirika la Afya Duniani (WHO) unaoendelea jijini Geneva Uswis kwa mikutano ya pembezoni kuelezea jitihada za nchi za uimarishaji wa huduma za afya. Akiwa kwenye Mkutano huo leo Februari 06, 2026, Dkt. Magembe amekutana na Mkurugenzi wa Programu wa Unitaid, Bwana Robert Matiru ambapo katika mazungumzo yao, Dkt. Magembe amesema mikakati na juhudi zinazotekelezwa na Serikali ya Tanzania, chini ya uongozi wa Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa) ikiwemo za kuweka mazingira wezeshi kwa wazalishaji wa bidhaa za afya. "Tumetumia fursa hii kukutana na shirika hili leo kwa sababu linafanya kazi na makampuni mbalimbali duniani kwa kuyaunganisha na utaalamu, mabenki na fursa za mikopo nafuu ili kuyawezesha kuanzisha viwanda vya bidhaa za afya zenye ubora na ushindani wa kimataifa," amesema Dkt. Magembe  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Programu wa Unitaid, Bwana Robert Matir...

WAANDISHI WATAKIWA KUANDIKA UCHUNGUZI NA UWAJIBIKAJI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Arusha. WAANDISHI wa habari za mazingira wa Kanda ya Kaskazini na Kati, wametakiwa kuandika habari za uchunguzi ambazo zinachochea mabadiliko ya sheria na sera na kuhimiza uwajibikaji. Wakitoa mada katika mafunzo ya waandishi wa habari za mazingira, yaliyoandaliwa na Mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu (THRDC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Wanahabari inayosaidia jamii za asili (MAIPAC), Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari nchini(UTPC), Kenneth Simbaya na Mkurugenzi wa MAIPAC, Mussa Juma wamesema wakati wa kuandika habari za matukio umepita. Simbaya amesema katika uandishi wa kisasa ni muhimu sana, habari ichochee mabadiliko ya sera na sheria badala ya kuandika matukio ya kila siku. "LHRC na MAIPAC wameandaa mafunzo haya, ili muandike habari za uchunguzi za mazingira ambazo zinachochea mabadiliko lakini pia mzingatie maadili," amesema Simbaya. Kwa Upande wake Juma, licha ya kuhimiza habari za uchunguzi ambazo zinaleta uwajibikaji kati...