Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 31, 2025

TAARIFA KWA UMMA

Picha
Gaza  ABU Obeida, anayejulikana kwa kuonekana akiwa amejifunika uso kwenye ujumbe wa video, alikuwa msemaji wa kikosi cha kijeshi cha Qassam na sauti kuu ya propaganda ya Hamas. Tangu kuanza kwa vita vya Gaza, Israel imewaua viongozi kadhaa wa Hamas, akiwemo Yahya Sinwar, anaetajwa kuwa mpangaji mkuu wa mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 kusini mwa Israel.  #Gaza #Israel #Hamas #AbuObeida #MiddleEastConflict Credit DW. 

JESHI LA ISRAEL LAFANYA MASHAMBULIZI USIKU KUCHA GAZA

Picha
JESHI la Israel limefanya mashambulizi ya usiku kucha kwenye maeneo yaliyoko Mjini Gaza kutokea angani na ardhini na kuharibu majumba na kuzilazimu familia zaidi kuondoka eneo hilo. #Gaza #Israel #evacuation

NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUTUMIKA MAGEREZA YOTE NCHINI

Picha
Matukio mbalimbali katika picha yakimuonesha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa matumizi ya nishati safi ya kupikia magerezani, iliyofanyika Agosti 30, 2025, Gereza Karanga, Kilimanjaro.

ABIRI AKAMATWA BAADA YA KUMPIGA NGUMI MUHUDUMU WA KWENYE NDEGE

Picha
POLISI wamemkamata abiria kutoka kwenye ndege iliyowasili kutoka Saudia kwenye uwanja wa ndege huko Heathrow mapema Alhamisi ya wiki iliyopita.  Polisi na Maofisa wa  Wazima Moto waliizingira ndege ya Saudia Airlines katika uwanja wa ndege wa Heathrow na kumkamata abiria wa kiume mwenye umri wa miaka 33 ambaye inadaiwa alimpiga ngumi mfanyakazi na kujaribu kufungua mlango wa ndege hiyo. Huduma za dharura zilikimbilia kwenye Boeing 787 muda mfupi baada ya kutua kutoka Jeddah majira ya saa 7 mchana ya Alhamisi. Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, ndege hiyo ilifunga breki kali kwenye barabara ya teksi kuelekea Terminal 4 baada ya tukio hilo, na kuwafanya marubani kuita usaidizi wa haraka. Ngazi ziliwekwa na maafisa walipanda ndege hiyo, iliyokuwa imebeba abiria kwenye Flight namba SV119. Picha zilizopatikana na gazeti la The Sun zinaonyesha angalau malori manne ya zima moto, magari sita ya polisi na ambulensi kadhaa kwenye eneo la tukio.