ABIRI AKAMATWA BAADA YA KUMPIGA NGUMI MUHUDUMU WA KWENYE NDEGE




POLISI wamemkamata abiria kutoka kwenye ndege iliyowasili kutoka Saudia kwenye uwanja wa ndege huko Heathrow mapema Alhamisi ya wiki iliyopita. 

Polisi na Maofisa wa  Wazima Moto waliizingira ndege ya Saudia Airlines katika uwanja wa ndege wa Heathrow na kumkamata abiria wa kiume mwenye umri wa miaka 33 ambaye inadaiwa alimpiga ngumi mfanyakazi na kujaribu kufungua mlango wa ndege hiyo.

Huduma za dharura zilikimbilia kwenye Boeing 787 muda mfupi baada ya kutua kutoka Jeddah majira ya saa 7 mchana ya Alhamisi.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, ndege hiyo ilifunga breki kali kwenye barabara ya teksi kuelekea Terminal 4 baada ya tukio hilo, na kuwafanya marubani kuita usaidizi wa haraka.

Ngazi ziliwekwa na maafisa walipanda ndege hiyo, iliyokuwa imebeba abiria kwenye Flight namba SV119.

Picha zilizopatikana na gazeti la The Sun zinaonyesha angalau malori manne ya zima moto, magari sita ya polisi na ambulensi kadhaa kwenye eneo la tukio.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.