Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 11, 2026

BAROZI MATINYI AKABIDHI HATI KWA RAIS WA ALGERIA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Algeria.  BAROZI wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare  Matinyi, amekabidhi hati za utambulisho wa kibalozi kwa Mhe. Rais Abdelmadjid Tebboune wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria katika hafla iliyofanyika kwenye Ikulu ya jijini Algiers, tarehe 10 Juni, 2026, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi utekelezaji wa majukumu ya kibalozi. Katika mazungumzo yao mafupi yaliyofuatia baada ya hafla hiyo, Mhe. Balozi Matinyi alimshukuru Mhe. Rais Tebboune, serikali na watu wa Algeria kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kudumisha ushirikiano wa kindugu wa nchi hizi mbili ambao umedumu kwa zaidi ya miongo sita. Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mazungumzo yake na Mhe. Rais Tebboune, Balozi Matinyi alisema kwamba walijadiliana namna ya kusonga mbele baada ya kufikia mafanikio mazuri katika sekta za ulinzi na elimu ya juu ili kuhakikisha watu wa nchi hizi wananufaika pia katika sekta zingine muhimu. Mh...

UNYONYAJI WA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI BADO WATAJWA KUWA CHANGAMOTO

Picha
Na Jasmine Shamwepu, Habari Kamili Blog-Dodoma.  MATUKIO ya unyonyaji, mishahara duni na ukosefu wa mikataba ya ajira yameendelea kutajwa kuwa miongoni mwa changamoto zinazoathiri ustawi wa wafanyakazi wa majumbani nchini, hali inayochochea wito wa kuwepo kwa hatua zaidi za kuwalinda. Hayo yameelezwa na wadau wa sekta ya ajira wakati wa mkutano wa kujadili utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Kazi za Majumbani wa mwaka 2025/26 hadi 2029/30 uliofanyika jijini Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Majumbani nchini, Zanini Athumani, amesema pamoja na umuhimu wa kazi za majumbani katika jamii, bado baadhi ya wafanyakazi wanakabiliwa na mazingira yasiyozingatia haki zao za msingi. Amesema changamoto hizo zinajumuisha kucheleweshwa kwa mishahara, kutokuwepo kwa mikataba ya kazi na kukosekana kwa mifumo madhubuti ya kushughulikia malalamiko wanayokumbana nayo. “Wafanyakazi wengi wa majumbani bado wanahitaji ulinzi zaidi ili waweze kufanya kazi zao kwa usalama na kupata stahiki zao ...