PET SCAN IANZE KUFANYA KAZI OCEAN ROAD- DKT SHEKALAGHE
Na. Lubango Mleka, Dar es Salaam. KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, ameuagiza uongozi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na mkandarasi anayesimika kifaa tiba cha PET Scan kuhakikisha wanakamilisha usimikaji wa kifaa hicho ndani ya muda waliokubaliana. Dkt. Shekalaghe ametoa agizo hilo Novemba 25, 2025, wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa utoaji wa huduma katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, jijini Dar es Salaam. “Tumekubaliana kwamba hadi siku ya Ijumaa, mkandarasi anatakiwa kumpatia Mkurugenzi wa Ocean Road uhakiki wa benki (Bank Guarantee) ili Mkurugenzi aweze kumlipa asilimia 75 ya malipo yake. Hii itamwezesha mkandarasi kufanya maandalizi ya kuhakikisha PET Scan inaanza kufanya kazi. Wataalam wamenishauri kuwa baada ya hapo tutahitaji siku 30 kwa ajili ya maandalizi ya mashine hiyo kuzalisha mionzi tiba kwa ajili ya kugundua kansa,” amesema Dkt. Shekalaghe. Aidha, amewahakikishia wananchi wanaofika hospitalini hapo kupata huduma, kuwa Serikali imenunua galimu ...