KANISA LA FPCT LAIPONGEZA SERIKALI KUSOGEZA HUDUMA ZA MOYO KWA WANANCHI




Na Mwandishi Wetu, Nkinga - Igunga.

KANISA la FPCT Jimbo la Nzega limeipongeza Serikali ya awamu 6 chini ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ujio wa Madaktari Bingwa Bobezi wa Moyo walioweka Kambi ya matibabu ya Moyo Hospitali ya Rufaa ya Nkinga Igunga.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Askofu Ezekiel Silasi wa Jimbo la Nzega alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Nkinga ili kuona jinsi huduma za kambi zinavyotolewa kwa wananchi.

"Ujio wao umeleta tija kubwa katika jamii yetu lakini kwa Kanisa la FPCT, tunasikia kuthaminiwa sana, binafsi kwaniaba ya Askofu Mkuu niwashukuru sana Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kuja hapa Nkinga kutuletea huduma hii lakini pia kuwapa uzoefu Madaktari wetu."

Ameongeza, "Ushirikiano huu uendelee kwa sababu Afya za watanzania zikiimarika hayo ndio maendeleo ya nchi yetu" amesema Askofu Silasi.

Bw.Omary Kalonga mkazi wa kata ya Magengati wilayani Nzega ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Nkinga kuwaleta Madaktari hao kwani ingewagharimu fedha nyingi kufuata huduma hizo Hospitali za Kanda.

Hospitali ya Rufaa ya Nkinga ni taasisi inayomilikiwa na Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania chini ya Askofu Mkuu Mch.Stevie Mulenga.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.