Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 29, 2025

RIPOTI YA FEDHA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA

Picha
Ripoti ya hivi karibuni kabisa ya Benki Kuu ya Tanzania inaonesha zaidi ya robo ya wale waliochukua mikopo binafsi mwaka 2024 waliitumia kununua magari na kugharamia matibabu.  Katika ripoti hiyo ya Uhimilivu wa Sekta ya Fedha, takwimu zinaonesha asilimia 14.7 ya mikopo ilikwenda kwenye matibabu na 14.2 ilitumika kununua magari. Ujenzi wa nyumba na kulipia masomo ni matumizi mengine makubwa yaliyofanywa na wale waliochukua mikopo binafsi mwaka uliopita. Je, wewe hukopa kufanyia nini?

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUWA MGENI RASMI MKUTANO MKUU WA WATUNZA KUMBUKUMBU NA NYARAKA TANZANIA.

Picha
Na. Mwandishi Wetu, Dodoma.  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) tarehe 27 Agosti, 2025 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dare s Salaam. Akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo leo jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema pamoja na kufungua rasmi mkutano huo, Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa pia ataendesha zoezi la harambee kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Maarifa kitakachokuwa na masijala ya mfano, kumbi za mikutano pamoja na ofisi za TRAMPA kinachotarajiwa kujengwa jijini Dodoma. Kufuatia mkutano huo wa kitaaluma, Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa Waajiri wote kuwaruhusu Watunza kumbukumbu ili waweze kushiriki kwani ni jukwaa muhimu la  kuwajengea uelewa wa majukumu wanayoyatekeleza ukizingatia kwa s...

CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA WA UBUNGE,

Picha
..MAKALLA MCHAKATO UMEVUNJA REKODI Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  BAADA ya kusubiriwa kwa hamu kwa muda mrefu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) hatimaye kimetangaza rasmi majina ya wagombea waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Tangazo hilo limetolewa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, katika Makao Makuu ya chama hicho jijini Dodoma. Makalla amesema kuwa kazi ya kuchambua na kupitisha majina ya wagombea ilikuwa kubwa kutokana na idadi kubwa ya waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali.  Amesema Kamati Kuu ya CCM ilifanya kazi hiyo kwa umakini na weledi ili kuhakikisha kila jina lililopitishwa linaakisi maadili, uwezo na utekelezaji wa sera za chama. “Wagombea walikuwa wengi sana, kazi ya kuandaa orodha haikuwa nyepesi. Tulihakikisha tunamaliza kwa usahihi mkubwa, kwa kuzingatia maoni na mapendekezo ya vikao halali vya chama,” alisema Makalla. Makalla aliwapongeza waombaji wot...