Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 7, 2026

PROF. SHEMDOE AKUTANA NA MKURUGENZI WA BENKI YA AZANIA KUJADILI MAENEO YA USHIRIKIANO

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma. WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amekutana na Mkurugenzi mtendaji Benki ya Azania Bi. Esther Mangenya na kufanya mazungumzo ya namna bora ya kushirikiana katika kuboresha utoaji wa huduma za afya msingi, elimu msingi na ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja miundombinu ya huduma nyinginezo za kijamii. Prof. Shemdoe alifanya mazungumzo hayo na Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya Azania hivi karibuni ofisini kwake Jijini Dodoma, alipomtembelea kwa lengo la kujitambulisha ili kujenga mahusiano mazuri ya kiutendaji yatakayowanufaisha wananchi waliopo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Katika kikao kazi hicho, Prof. Shemdoe na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bi. Esther Mangenya wamekubaliana kujenga mahusiano mazuri ili wananchi wanufaike na mchango wa Serikali na benki hiyo katika kuboresha miundombinu ya utoaji wa huduma za kijamii. Kwa kutambua mchango wa taasis...

UPENDO NA MAELEWANO VYATAJWA KUWA MSINGI WA AMANI NCHINI

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Dar Es Salaam. ADAM Seleman, Mkazi wa Msongora Jijini Dar Es Salaam amesema tafsiri halisi ya amani ni pamoja na kuelewana na kupendana miongoni mwa Watanzania, akihimiza upendo na maelewano kama msingi wa kudumisha amani na utulivu nchini. Bw. Selemani amebainisha hayo leo Jumamosi Februari 07, 2026 wakati akizungumza na mwandishi wetu wa habari kuhusu umuhimu wa amani kwa ustawi na maendeleo, akisema familia, Jamii na Nchi yoyote inahitaji amani na utulivu ili kuweza kutimiza majukumu na wajibu walionao. "Maana halisi ya amani ni ile hali ya mtu kuwa na uhuru wa kufanya jambo ambalo linaruhusiwa Kikatiba na pia amani tafsiri yake ni upendo, tukipendana ndio amani yenyewe kuanzia ndani ya nyumba. Nawaomba sana tuendelee kushikamana na kudumisha hiki tulichonacho kwani sisi nchi yetu ni kisiwa cha amani." Amesema Bw. Selemani.

AMANI INATUPA UHURU WA KUJIENDELEZA KIUCHUMI- NIACHIENI

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dar Es Salaam. UWEPO wa amani katika Taifa kumetajwa kama miongoni mwa rasilimali muhimu zinazohitajika ili kufanikisha malengo na mipango ya mtu mmoja mmoja, Familia, Jamii na Taifa kwa ujumla, Wito ukitolewa kwa Watanzania kuilinda na kudumisha amani. Kauli hiyo imetolewa na Bw. Ramadhan Mohamed Niachieni, Mkazi wa Mtaa wa Mkera, Kata ya Msongora Jijini Dar Es Salaam, akisisitiza kuwa amani ndiyo yenye kuleta maendeleo nchini hivyo kila mmoja anawajibika kuilinda kwa ustawi na maendeleo yetu binafsi. "Amani ina tija sana katika nchi yetu ikiwemo maendeleo ya kila hali kutokana na uhuru wa kufanya shughuli zetu za kiuchumi. Naomba sana tuilinde ili tusiharibikiwe kama wengine na ili tupate fursa ya kuijenga nchi yetu." Amesema Bw. Niachieni. Mwananchi huyo anaungana na maelfu ya wananchi wengine ambao wamekuwa wakisisitiza kuhusu ulinzi wa amani na kuwakataa wote wenye kuhatarisha amani nchini, wakirejea athari za kiuchumi na kijamii zilizojitokeza waka...

WITO WATOLEWA, JITIHADA ZA PAMOJA UDHIBITI WA SILAHA HARAMU NCHINI

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dar Es Salaam. KAMATI ya udhibiti na usimamizi wa silaha  imetakiwa kujikita katika utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya silaha haramu ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya silaha haramu. Kauli hiyo imetolewa wakati wa ufungaji wa kikao cha kwanza cha mafunzo cha kamati ya udhibiti na usimamizi wa silaha, kilichofanyika kwa siku tatu Jijini Dar Es Salaam, wajumbe wakikubaliana kuwa ikiwa elimu itatolewa na jamii ikaelewa madhara ya kusambaa kwa silaha haramu, nchi itakuwa salama. Mapema akifunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, IGP Camillus Wambura amesema wajumbe wa kamati hiyo ni watu makini na wameonesha kuwa watakuwa msaada mkubwa katika kutekeleza majukumu yao kutokana na kuwa wabobezi katika nyanja tofauti kutoka Serikalini na sekta binafsi. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini na Mrajisi Mkuu wa Silaha DCI Ramadhan Kingai alisema wataendelea kuchukua hatua kali kwa wamiliki...